Matokeo ya utafiti kuhusu utumiaji wa dawa za kusaidia kupata usingizi

 
Ripoti ya uchunguzi wa utafiti kuhusu matumizi ya dawa za kusaidia kupata usingizi yameonesha kuwa wanawake (5%) huhitaji kutumia zaidi dawa ya kusaidia kupata usingizi kuliko wanaume (3.1%)

Ingawaje utafiti huu umefanywa nchini Marekani kwenye mazingira na mambo mengine yanayoweza kuwa tofauti na kwingineko ulimwenguni, bado takwimu hizi zinaonesha umuhimu na kutoa msaada kwa watu ambao husumbuliwa na kukosa hata lepe la usingizi kwani watajifahamu kuwa hawapo wenyewe katika tatizo hili na pia wataweza kujinganisha umri wao na umri wa waliotafitiwa na kuona kama wapo (au ndugu zao wapo) katika kundi la waathirika zaidi.

Kwa mfano, utafiti huo uliofanywa kati ya mwaka 2005 hadi 2010 kabla ya ripoti yake kutolewa sasa,
umetambua kuwa Wamarekani milioni tisa walitumia dawa za kusaidia kupata usingizi ndani ya mwezi mmoja tu uliopita.

Kati ya hao, asilimia 7 ya watu wenye wenye umri wa zaidi ya miaka 80 walihitaji dawa hizo ili kupata usindizi. Kundi lililotumia kiasi kidogo cha dawa hizo  ni lile la umri wa kati ya miaka 20 hadi 39 (asilimia 1.8 ya watafitiwa).

Wazungu walitumia zaidi dawa hizo zaidi ya watu weusi au wenye asili ya Mexico.

Mapema mwaka huu, mamlaka ya Chakula na Dawa nchini humo ilitahadharisha dhidi ya matumizi ya dawa za kusaidia kupata usingizi kama vile Zolpidem (Ambien), kwani kiasi fulani cha dawa hiyo kinachobaki mwilini mtu anapoamka, kinaweza kuendelea kumsababisha awe na usingizi bila kujitambua na hivyo kusababisha madhara hasa ikiwa mtu huyo atakuwa dereva au anayefanya kazi katika mashine. Madaktri kwa sasa wanashauriwa kuwapa wahitaji dawa kwa kiwango cha chini kabisa cha dawa hiyo (5 mg), kuliko kile kilichokuwa kinatolewa hapo awali ambacho ni mara mbili ya cha sasa.

---

Ni vyema kabla ya kukimbilia dawa, mtu akajitahidi kutatufa usingizi kwa njia zisizohitaji dawa kama vile kunywa maziwa ya moto glasi moja nusu saa kabla ya kulala, kusikiliza muziki wa taratibu (ikiwezekana usio na maneno – instrumental) kusoma kitabu, kutokunywa vinywaji (mathalani chai, kahawa, soda, vinywaji vya kuongeza nguvu n.k.,) saa moja kabla ya kulala na jitahidi kutokwenda kitandani na hasira au mawazo yanayohitaji kutumia akili sana kupata utatuzi (akili leo imeshindwa kupata jawabu hivyo ipumzishe ili ipate nguvu mpya ili kesho kukikucha huenda utapata jawabu la kuyashughulikia, kumbuka matatizo hayakukupata wewe peke yako na hayaishi duniani).

Jaribu kupata usingizi kwa kusugua nyayo za miguu ukiwa kitandani tayri kwa kulala, funika nyayo zako kwa kipande cha shuka, khanga au taulo la joto, kuhesabu kuanzia 1000 kushuka chini hadi 0, kuwaza mawazo mazuri mathalani ya kukumbuka nyakati za furaha, matazamio mema…..n.k. Njozi njema!

Post a Comment

Previous Post Next Post