Mama
mzazi wa marehemu Albert Mangwea, Denisia Costantine Mangwea,
amelazimika kuzungumza na kuthibitisha kuwa ni kweli alipewa fedha na
Mwana FA aliyeahidi kutoa asilimia 15 ya fedha iliyopatikana kwenye show
ya The Finest, June mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuzuka tuhuma kuwa Mwana FA ambaye jina lake ni Hamis Mwin’juma hakutimiza ahadi hiyo.
Akiongea na gazeti la Mwananchi la leo MwanaFA alikiri kutoa ahadi hiyo.
“Nakiri kukosea jambo moja, nilipoahidi, niliongea na wanahabari
lakini wakati wa kutoa, nilitoa bila kutangaza, na hii kutoa jamani ni
moyo, haina haja kumtangaza mtu kwa kuwa umemsaidia au umempa pole,”
Mwana FA ameliambia Mwananchi.
Aliongeza shilingi milioni 19.5 alizoingiza, alitoa shilingi milioni
tatu na kuzikabidhi kwa mama yake Ngwair kwa kuziingiza kwenye akaunti
yake ya benki ya Exim. Gazeti la Mwananchi limedai kuwa liliamua kwenda
hadi Morogoro kwa mama huyo kuthibitisha kama kweli alipokea fedha hizo.
“Kabla hata ya arobaini, aliweka benki kisha akaja na mwenyewe,
hakuna na waandishi kama wanavyofanya wenzake, alikuja mwenyewe
tukaongea, na mara kwa mara tunawasiliana, wanataka kumtia doa kijana wa
watu ni muungwana sana,” Mama huyo aliliambia Mwananchi.
Ili kuthibitisha mama huyo alitoa risiti aliyokabidhiwa na MwanaFA
ikionesha kiasi cha fedha alichotoa na tarehe halisi ambayo fedha hizo
ziliwekwa kwenye akaunti yake.
“Naomba kwa niaba ya familia niwathibitishie alitoa na mngemwacha
kijana wa watu aendelee na shughuli zake, kwani alitoa kwa nia njema na
ndiyo maana hakutaka kuitangaza sana,” aliongeza.
Source: Mwananchi
إرسال تعليق