Mama huyu kakamatwa kama mhamiaji haramu na kupelekwa Ubalozi mdogo wa
DR Congo uliopo Manispaa ya Kigoma. Amezaliwa Tanzania, amesomea
Tanzania, baba yake Mtanzania, babu yake Mtanzania na ndugu zake wengine
Watanzania na hawakukamatwa. Amekamatwa akitoka kuchota maji ziwani
Tanganyika. Malalamiko yake nimeyafikisha kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Post a Comment