Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu
na Bunge) Mhe. William V. Lukuvi (MB) kuanza ziara rasmi leo tarehe
16 hadi 19 Septemba, 2013 katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi anatarajiwa kutembelea
baadhi ya vituo vya Ununuzi wa Mahindi kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye
Maghala ya National Food Reserve Agency (NFRA), Maghala ya NFRA ya kuhifadhi
chakula, atapokea taarifa ya Utekelezaji kuhusu Mradi wa Miundo Mbinu
ya Masoko na Uongezaji wa Thamani (MIVARF) katika maeneo yanayotekeleza
mradi huu.
Vilevile Mhe. Lukuvi atapokea Taarifa ya Utekelezaji
wa Miradi yote ya Maendeleo ikiwemo Miradi itokanayo na ahadi za Mhe.
Rais na Miradi itokanayo na Ilani ya Chama Tawala pamoja na Miradi inayofadhiliwa
na Taasisi mbalimbali Mkoani humo
Post a Comment