Mtazame mtoto wa miaka 12 wa Brazil akiimba ‘We Are The World’ ya Michael Jackson ‘Live’ (Video)


Wow wow wow, ndio neno la kwanza lililonitoka baada ya kutazama video hii ya mtoto Jotta A kutoka Brazil mwenye kipaji cha hali ya juu akiimba ‘live’ wimbo wa marehemu Michael Jackson ‘We Are The World’.
Cha kusisimua zaidi ni jinsi alivyoutawala wimbo jukwaani kwa hisia na kujiamini na kubwa zaidi ni kuwa anaimba live huku akipigiwa vyombo pamoja na kusindikizwa na waitikiaji, ‘this kid is amazing’!
Jina lake halisi ni José Antônio Viana de Hollanda, aka Jotta A aliyezaliwa Oktoba 8, 1998 huko Brazil. Alianza kwa kuimba gospel akiwa na miaka 6. Kutokana na uwezo mkubwa wa kuimba alionao amekuwa akiwavutia watu wengi kiasi kwamba video zake za Youtube zimefikisha hits zaidi ya 30,000.
Watu wanamfananisha sana na Michael Jackson kutokana na uwezo wake wa kuimba.

Post a Comment

Previous Post Next Post