RAIA mmoja wa nchi ya Canada amekamatwa nchini
Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo
bandia la ujauzito alimokuwa ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Mwanamke huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto,
alihojiwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Bogota aliyemshuku na
kumuuliza alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua.
Alijibu kwa ukali mno, hali iliyomfanya afisa huyo kumshuku sana na
hivyo kumfanyia ukaguzi zaidi. Afisa huyo aligusa tumbo lake na kuhisi
ilikuwa baridi mno na gumu sana ndipo askari hao wakaamua kumkagua
zaidi.
walimkuta na dawa za kulevya zilizokuwa zimefungwa ndani ya tumbo
bandia la mimba ambayo mwanamke huyo alikuwa amevaa kwa kufunga tumboni.
Inasemekana kuwa alisema ana miezi saba ya ujauzito lakini baada ya
polisi kumkagua walimpata na Cocaine kilo mbili iliyokuwa ndani ya
vipochi viwili.
Mwanamke huyo atashtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa madawa ya kulevya
na huenda akafungwa jela kwa miaka mitano au nane. Mwaka huu pekee
karibu watu 150 wamekamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege
wa Bogota. Karibu thuluthi moja ya waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni,
kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini Colombia.
-BBC
إرسال تعليق