Mwanasiasa kunyongwa Bangladesh

Abdul Quader Mollah
Mahakama ya Juu nchini Bangladesh imemhukumu kifo mwanasiasa wa kiislamu aliyepatikana na hatia ya mauaji ya halaiki wakati wa vita vya Ukombozi kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.
Abdul Quader Mollah wa chama cha upinzani cha Jamaat E Islami alihukumiwa maisha na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita hapo mwezi Fabruari.
Wakili wake amesema hii ndio mara ya kwanza hukumu ya maisha imeongezwa na kua kunyongwa.
Hukumu ya awali ilichochea maandamano ya wafuasi wa chama chake ambao wamesema hukumu dhidi ya Mollah imechochewa kisiasa.
Lakini wapinzani wake wanasema kuwa hukumu hiyo ni dhaifu mno.
Maelfu walifanya maandamano kote nchini wakitaka Mullah ambaye alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya halaiki wakati wa vita vibaya zaidi vya kupigania uhuru anyongwe.
Maandamano hayo yalichochea bunge kufanya mageuzi ya sheria ambayo yanaruhusu serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wowote ulioafikiwa na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita nchini humo.
- bbc

Post a Comment

Previous Post Next Post