
Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake.
Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anaetafutwa
na polisi.
Polisi wa kituo cha kawe akiukagua mwili wa marehemu Yusta Mkali.
Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya
Mwananyamala.
Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa
ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
---
Na Mwandishi wetu.
Mkazi wa Kawe
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi
kwa mahojiano baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta
Mkali.
Mauaji hayo
yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji hayo
kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius
Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwa uchunguzi wa awali
mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia(leo) jana.
“Yusta
ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika
mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani
yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.
Wambura
alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
Naye Mtoto wa
dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye
ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi
chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo
alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.
“Ilikuwa
majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama
ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta
mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio
nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema
kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.
Marehemu
Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma
Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
إرسال تعليق