POLISI WAAMBIWA KUTUMIA RASILIMALI ZILIZOPO KUBORESHA HUDUMA KWA JAMII


MAAFISA  wanadhimu, waasibu pamoja na  maafisa mipango wa Jeshi la Polisi wametakiwa
kuongeza kasi  ya   Usimamizi wa rasilimali  ndani ya Jeshi la Polisi  ili kuboresha
utendajikazi wao na kutoa huduma bora kwa Jamii.

Hayo yalisemwa na Naibu katibu MKuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya NChi, Mwamini 
Maleme Wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maafisa wanadhimu, waasibu na maafisa
mipango wa mikoa na Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi kinachoendelea mkoani
Kilimanjaro katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA).

Mkutano huo hufanyika Kila mwaka ambao una lenga kutathimini  hali ya utendaji wa
jeshi la polisi na usimamizi    Wa rasilimali za Jeshi la Polisi pamoja na kuboresha
usalama wa raia na Mali zao ili kupunguza malalamiko  na kuongeza kasi ya utoaji  wa
huduma bora kwa wananchi.

Aidha,  alisema  kuwa mkutano huo utawawezesha watendaji wote wa Jeshi la polisi
kuweka mipango ya pamoja itakayo saidia kupunguza uhalifu na kuimarisha amani na
utulivu nchini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa sera, mipango na bajeti ya Jeshi la
Polisi.

Kwa upande wake, Kamishina wa utawala na rasilimali wa Jeshi la Polisi (CP) Clodwig
Mtweve ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo, alisema kuwa mkutano  huo
utawawezesha watendaji  kuboresha mikakati na mipango ya kuimarisha  usalama wa raia
na Mali zao pamoja na  kuzuia ajali barabarani ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu 
na maadili ndani ya Jeshi la Polisi. 

Alisema kuwa hivi sasa Jeshi hilo linaendelea na mkakati wake wa kufikisha huduma ya
usalama hadi ngazi ya familia, mkakati  huo unatekelezwa kupitia Mradi wa Askari
Tarafa ambao jukumu Lao kubwa ni Kushirikiana na Jamii katika kutatua kero
mbalimbali za kiusalaam ndani ya jamii.

Naye Mhasibu mkuu wa Jeshi la polisi Bw. Frank Msaki  alitoa shukrani  kwa niaba ya 
ya Jeshi la Polisi na kuwataka wajumbe kutumia mkutano huo Kama fursa ya kuboresha
utendaji katika sehemu zao ili kuleta matokeo makubwa.
SOURCE:Na Tamimu  Adam, Jeshi la Polisi  Moshi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post