Sam Wa Ukweli aeleza sababu za ukimya wake na ujio wa project yake mpya, amtuhumu Papaa Misifa kwa kumnyamazisha na kumhujumu

sam2
Sam akiwa studio za Defatality
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Sam wa Ukweli aliyehit sana kipindi flani kwa ngoma zake mbili ‘Sina raha’ na ‘Hata kwetu wapo’, amefunguka exclusively kupitia bongo5 kuhusu sababu zilizompelekea huwa kimya kwa muda mrefu na kutoyagusa tena matawi ya nyimbo hizo mbili.

Kuhusu sababu za ukimya wake na kama ameshafanya kazi kadhaa na Mensen Selekta
Jana mwimbaji huyo aliweka picha kwenye instagram akiwa katika studio za DeFatality akifanya kazi baada ya kimya kirefu .
“Hii ni mara yangu ya kwanza nafanya kazi na Mensen Selekta, na kikubwa ambacho kilichokuwa kimenikwamisha ni kwa sababu ile management niliyokuwa nafanya nayo kazi zamani, kuna some problems zilitokea baina yangu mimi na wao kwa sababu kuna taratibu tulizokuwa tumepanga mimi na wao lakini walienda kinyume na mimi kwa hiyo nikawa siwezi kusimama kwa hiyo nikastopisha.
Sam aliendelea kusema “ Kwa hiyo swala la mkataba likawa limenibana nikawa nimeweka vikwazo kuwa siwezi kufanya kazi na mtu yeyote mpaka nimalize ule mkataba (Papaa Misifa). Kwa hiyo hivi sasa mkataba umekwisha niko huru naweza kufanya kazi na mtu yeyote na ndo maana jana nimeenda studio nikafanya kazi na Mensen Selekta, na ni kazi nzuri naamini itafanya poa.”
sam defatality studio
Kuhusu Wimbo ambao ameurekodi kwa Mensen Selekta na ujumbe wake
“Hii ni ngoma moja ambayo nimeifanya pale , na ngoma inaitwa ‘Umetumwa’ , na kitu ambacho nimezungumzia humo ndani ni kama partition tatu tofauti. Kwanza nazungumzia kuhusu mahusiano ya watu ambayo mtu anataka kuyaingilia japokuwa hajui wameanzia wapi, pili nimezungumzia kuhusu Muziki kwa sababu mimi na wewe tunaweza kuwa wanamuziki halafu akawepo mtu ambae anataka kututumia kwa kutugombanisha kwa maslahi yake yeye lakini akatuumiza mimi na wewe ikawa mimi na wewe tunavurugana halafu anapata mafanikio yeye. Tatu nikawa nazungumzia maisha tunayoishi sisi inawezekana kwenye nyumba, majirani ama nyumba za kupanga inawezekana nyie mkawa mnakaa sehemu moja na na mnaelewana halafu ikatokea mtu akaoa mwanamke ama hata akaleta mtoto ambae akaanzisha chokochoko kuwagombanisha nyinyi. Hata wewe unaweza kumwambia mtu ‘mi sina ugomvi na wewe, vipi bwana umetumwa.”
Kuhusu Mahusiano yake na Producer wake ‘Kisaka’ na chanzo cha ugomvi wake na Papaa Misifa
“Kwa Kisaka nilikuwa nafanya nae kazi tu kama production, kama marafiki na ndugu, ni mtu ambae nimefanya nae kazi kwa muda mrefu lakini hatukuwa na mkataba wowote, na ndo maana first time nilifanya nae ‘Sina Raha’ na ‘Hata Kwetu wapo’, project ambayo ilikuwa chini usimamizi wa Kisaka. lakini baadae nikampata mtu anaeitwa Papaa Misifa ambae ana kampuni ya Aljazeera Entertainment, na first time ilikuwa ikifanya kazi na Diamond, Diana na Timbulo, so jamaa akakaa akasema tufanye kazi kwa kuwa nina kipaji kizuri na uwezo mzuri, nikaona sawa.
Lakini sikuwa najua lengo lake, labda lengo lake lilikuwa anataka ni-drop kwa kuwa kuna mtu ambae nilikuwa nacompete nae, ama alitaka nipotee tu kwenye huu muziki manake mtu mwingine anaweza kuwa anakutafuta sana akakukosa akaamua kukutafuta huku. Kwa hiyo kwenye project yote wimbo ambao tuliufanya ni ‘Samaki’, na video pekee yake tulizungushana takribani mwaka mzima,akawa ananiambia tayari ameshamlipa pesa Adam wa Visual lab na kumbe uongo, kwa hiyo kulikuwa na uongouongo, kwa hiyo lilikuwa la kwanza. La pili , tulikuwa tunafanya show Kahama na kukawa na mazingira ya kututapeli ndo tukacomplain tukagombanagombana lakini tukawa tumesuluhisha yakawa yameisha.
Sam aliendelea kufunguka, “Kwa hiyo ni mtu ambae anafanya vitu ambavyo viko wrong, alikuwa anaenda Push Mobile ambapo ngoma yangu ya ‘Sina Raha’ na ‘Hata kwetu wapo’ zilikuwa zinafanya vizuri, akawa anaenda anachukua pesa bila kunambia wakati hizo akaunti zilikuwa hazimhusu zilikuwa zangu binafsi. Kwa hiyo nilikuwa nikipigiwa simu na Push Mobile kuwa pesa zimetoka nikienda nakuta yeye ameshachukua. Kwa hiyo nikaona mtu kama huyo mkifanya show mkapata hata million Ishirini anaweza kukuletea majambazi home, kwa hiyo sio mtu mzuri kufanya nae kazi na mimi nikamwambia bwana mimi sitaki kufanya kazi na wewe tena, akanambia hili swala litakuwa gumu we kama unataka kuachana na mimi subiri mpaka mkataba uishe”.
Kuhusu Project zake zinazokuja na kama atasimama mwenyewe au na manager mpya
Sasa hivi nimeamua kusimama mimi kama mimi na naandaa Project yangu ni kama mixtape, inayoitwa “Come Back Sam wa Ukweli, Mjini Kimenuka”, na kuna ngoma yangu ambayo nimeiachia nikiwa na Rich Mavoko na Z Anton, na baada ya hiyo zitafuata ambazo nimefanya na maproducer mbalimbali akiwemo Man Walter, Kwa Mazoo, Mensen Selekta, na wengine wengi yaani nafanya na producer yoyote, niko huru.
Kuhusu alichokikosa baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu
“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwamba nina afya nzuri, lakini nachojutia hasa ni kwamba watu kumiss ladha yangu kwa sababu ni mtu ambae nina madini mengi ambayo yanataka kumwagika ila kuna watu ni kama wameyafungia hivi.
Kitu kingine nachokijutia ni ‘Happiness’ kwa kuwa nilikuwa ni mtu mwenye furaha naechat na watu vizuri na nini, lakini pia kukaa kimya kwenye huu muziki kuna baadhi ya watu wako kama vile wamenisahau lakini wadau, mashabiki muendelee kusapoti muziki wangu Sam wa ukweli nimesimama tena upya, Mungu pekee ndiye anatakiwa aabudiwe na kushukuriwa kwa kufanaya hadi leo mimi niko hapa”.

Post a Comment

Previous Post Next Post