Timu zinazoshiriki michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars zawasili nchini Nigeria

 Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika .Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel Bi Lilian Kibiriti
 Kikosi cha timu ya wasichana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. (mwenye shuti)  ni kocha wa timu hiyo Rogacian Kaijage . 
Kikosi cha timu ya Airtel Rising stars  wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars ya Afrika  inayozinduliwa rasmi jana (jumatatu) Nchini Nigeria na kushirikisha timu kutoka katika nchi 17 barani Afrika
========  ======  ========
Timu zinazoshiriki michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars zawasili nchini Nigeria
·      michuano hiyo inafanyika  Lagos, Nigeria kuanzia 16 hadi  22 September 2013.
Timu zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana  katika viwajnja vya Agege. michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji guru wakiwemo Rober Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal
Timu ya Zambia ilikuwa yakwanza kutua siku ya Ijumaa ikifatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. timu ya mabigwa watetezi kutoka Niger ilitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed International  siku ya jumamosi  mchana pamoja na timu kutoka Congo Brazzaville
kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve na timu nyingine zinategemea kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza siku ya jumatatu
michuano ya Airtel Rising stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji  huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa
kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria bwana Segun Ogunsanya
aliongeza "wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote"
michuano ya Airtel Rising stars itafanyika nchini lagos Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 septemba 2013. wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika clinic  itakayosimamiwa na makocha wa Manchester united inayotegemea kufanyiaka mwaka kesho April 2014 nchini   Lubumbashi (Democratic Republic of Congo).

Post a Comment

Previous Post Next Post