
SIMBA SC imeonyesha ni tishio msimu huu baada tya kushinda mabao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku mshambuliaji Mrundi, Amisi Tambwe akifunga mabao manne peke yake.
![]() |
Amisi Tambwe akishangilia moja ya mabao yake Taifa leo |
Mabao mengine ya Simba leo yamefungwa na kinda mzalendo, Haroun Athumani Chanongo, huku wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wakilazimishwa sare ya 1-1 na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati Uwanja wa Chamazi, Ashanti United imevuna pointi ya kwanza baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji Azam FC. HABARI ZAIDI ITAFUATIA.
Matokeo mengine
إرسال تعليق