Ismail Jussa Muwakilishi – Mji Mkongwe
---
Kwa
mara nyengine tena leo hii (jana)kumetangazwa kutokea tukio la kumwagiwa acid
ambapo imeelezwa jioni hii(jana) Padri Joseph Magamba amemwagiwa acid maeneo
ya Sunshine Internet Cafe hapo Mlandege, mjini Zanzibar. Binafsi nalaani
vikali kitendo hicho cha kinyama na cha kishenzi kabisa.
Juzi tu Jumatano nilisoma katika gazeti la Mwananchi tukio la mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi Christian Msema wa Mburahati, Dar es Salaam kumwagiwa acid na watu wasiojulikana waliokuwamo kwenye bajaj.
Matukio haya ni ya kinyama na ya kutisha na yanaonekana kushika kasi kila uchao. Bahati mbaya licha ya Polisi kutangaza operesheni maalum ya kutafuta kile walichokiita mtandao wa acid hakuonekani mafanikio yoyote.

Hivi uwezo wa uchunguzi wa Jeshi la Polisi umeshuka kiasi hichi? Na kwa nini hadi leo Serikali haijapiga marufuku uuzaji au upatikanaji mwengine wa acid ambao unaonekana kufanyika kiholela kiasi cha kupatikana kirahisi na kutumika kufanyia uhalifu kiasi hichi?
Yeyote au kikundi chochote kilicho nyuma ya matukio haya kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kusakwa ili kuchukuliwa hatua kali dhidi yao.
Ismail Jussa
Muwakilishi – Mji Mkongwe
Post a Comment