Na Boniface Wambura, TFF
TEMEKE, MJINI MAGHARIBI KUCHEZA NUSU FAINALI COPA
Temeke
na Mjini Magharibi zinapambana kesho (Septemba 13 mwaka huu) katika
mechi ya nusu fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 15 itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
jijini Dar es Salaam.
Timu
hizo zimetinga hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao za robo fainali
ya michuano hiyo zilizochezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) asubuhi kwenye
uwanja huo huo.
Wakati
Temeke imetinga hatua hiyo baada ya kuilaza bao 1-0 Iringa lililofungwa
dakika ya 18 na Ramadhan Mohamed, Mjini Magharibi imeing’oa Mtwara kwa
ushindi wa bao 1-0.
Robo
fainali nyingine zinachezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) jioni kwa
Kilimanjaro kuvaana na mabingwa watetezi Morogoro huku Arusha
ikioneshana kazi na Ilala.
TFF YATOA ITC KWA WAWILI, MAULID RUKSA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) kwa Watanzania wawili kucheza mpira wa miguu nchini Afrika Kusini.
Wachezaji
hao; Robert Kobelo na Mohamed Ibrahim wamepewa hati hizo baada ya
kuombewa na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kama wachezaji
wa ridhaa ili wajiunge na klabu ya Cacau United ambayo timu yake
inacheza Ligi Daraja la Pili katika Wilaya ya Cacau.
Naye
mchezaji Said Maulid aliyejiunga na Ashanti United akitokea nchini
Angola msimu huu amepata ITC ambayo sasa inamwezesha kuchezea timu hiyo
katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoingia mzunguko wake wa
tatu keshokutwa (Septemba 14 mwaka huu).
MVELLA AJIONDOA KWENYE UCHAGUZI TFF
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Eliud Mvella amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika
Oktoba 27 mwaka huu.
Mvella
amemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu
Mbwezeleni akielezea uamuzi wake huo pamoja na mambo mengine umetokana
na kile alichodai kuwa Kamati hiyo haikumtendea haki kwa kumwondoa.
Mbwezeleni
amekiri kupokea barua hiyo, na kuongeza kuwa licha ya uamuzi huo wa
Mvella aliyekuwa ameomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia
Kanda Namba Saba ya mikoa ya Iringa na Mbeya, bado suala lake
litasikilizwa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.
Kamati
ya Mbwezeleni ilimuondoa Mvella katika kinyang’anyiro hicho kwa
kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective
responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya
Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye
muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa.
FDL SASA KUPIGWA UWANJA WA KAWAWA
Mechi
za nyumbani za timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoko Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) sasa zitachezwa katika Uwanja wa Kawawa badala ya ule wa
Lake Tanganyika.
Uamuzi
wa kuhamishia mechi hizo Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji umetokana na
Uwanja wa Lake Tanganyika kutumiwa na Serikali katika Operesheni Ondoa
Wahamiaji Haramu inayoendelea nchini kwa sasa. Uwanja huo hivi sasa
unatumika kuhifadhi wahamiaji hao
إرسال تعليق