African Star Entertainment – ASET ikishirikiana
na studio ya Fleva Inc Audio
Records and Video Production Pamoja
na Makubi Sports Promotion imeandaa Tamasha la vipaji vya Wasanii wa fani mbalimbali
za sanaa kwa Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kutoka na kufanikiwa
kupitia sanaa zao, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Octoba ambalo litaitwa Tamasha
la Vipaji 2013.
Ndugu
Waandishi , Malengo mahsusi ya Tamasha la Vipaji 2013 ni kuvionesha vipaji mbalimbali vya Wasanii
ambao bado hawajapata fursa ya kuonekana
pia kuhamasisha, kuendeleza na kulinda
vipaji vya wasanii hao ili vipawa
hivyo viwe ni sehemu ya nyenzo muhimu ya ajira za uhakika katika maisha ya vijana mbalimbali ambao
wamejiingiza katika taaluma ya sanaa. Tamasha hili pia litasaidia ukuzaji wa
ajira za Wasanii mbalimbali wataojitokeza.
Ndugu
Waandishi, walengwa
wakuu wa Tamasha la Vipaji 2013 ni
Wasanii wa Maigizo ya jukwaani
(Matangazo , Filamu & Tamthilia),Wasanii wa Vichekesho,Wasanii wa Muziki
Bongofleva (R & B, Raga, Hiphop n.k),Wasanii wa Kupiga na kucheza Ngoma za
Asili,Wasanii wa kucheza muziki wa Wasanii wa ndani au nje ya nchi,Kucheza show
za nyimbo mbalimbali za ndani na nje Kuigiza Sauti za watu mbalimbali
walio maarufu wa hapa Tanzania,Kuigiza kazi za Watangazaji maarufu wa vipindi
vya Radio na Televisheni vya Tanzania.
Wasanii wa Ubunifu wa michoroWasanii
wenye vipaji vya utangazaji wa vipindi vya radio na televisheni,pamoja na wale
wa Sanaa za maonesho ya mavazi
Ndugu
Waandishi, Wasanii
wataofanya vizuri katika tamasha hilo wapata fursa ya kufanya kazi (lebo) na
Studio ya Fleva Inc Record, pia kushiriki katika kazi zinazoandaliwa na ASET
ikiwemo filamu, tamthilia kuimba ,kucheza dance n.k. Pamoja na pia
tunakaribisha kampuni /taasisi mbalimbali kusaidia kufanikisha tamasha hili
pamoja na kuwasaidia Wasanii hawa
kufikia malengo
Ndugu
Waandishi, Fursa
hii ni adimu kwa Wasanii wengi hivyo Wasanii wanaohitaji kushiriki wafike Ofisi za ASET au Fleva Inc
Studio zilizopo Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kwa ajili ya Kujiandikisha, mwisho wa
kujiandikisha ni tarehe 30 Septemba 2013
saa kumi jioni,tamasha linatarajiwa kufanyika 21 Octoba 2013 katika Ukumbi wa
Vijana Hall uliopo Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Nawashukuru kwa usikivu
wenu tunaomba ushirikiano.
W.R
MAKUBI
Project
Meneja
Kwa
Niaba
ASHA BARAKA
Mkurugenzi
ASET/FLEVA
INC RECORDS.
إرسال تعليق