Na Nathaniel Limu
JUMLA
ya wanafunzi 22 wa shule tatu za msingi wilaya ya Ikungi mkoani
Singida,’wamebambwa’ wakiwa kwenye vyumba vya kufanyia mtihani wa taifa
darasa la saba,huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.
Wanafunzi
hao na idadi yao kwenye mabano walikuwa kwenye shule ya msingi
Muhintiri (2),Iglansoni (16) na Kinyampee (4) tarafa ya Ihanja wilaya ya
Ikungi.
Wakati
kwenye shule ya msingi Mnyange tarafa hiyo hiyo ya Ihanja mwanafunzi
mmoja wa kike hakufika kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
hakuhudhuria kufanya mtihani huo kwa kile kilichodaiwa tayari
ameishaozwa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Protace Magayane,aliyekuwa akikagua
maendeleo ya zoezi la kufanya mtihani huo katika siku yake ya mwisho
juzi, aliagiza wazazi wa mwanafunzi huyo wa kike ambaye hakufanya
mtihani,wachukuliwe hatua stahiki za kisheria haraka iwezekanavyo.
Baadhi
ya wasimamizi akiwemo Ernest Mahendeka wa shule ya Kinyampembee, Rebeca
Julius wa Muhintiri na Salum Jafari wa Iglanson wamesema ilibidi wajaze
fomu maalumu kulingana na maelekezo kabla ya kuwaacha waendelee na
mtihani kulingana na jinsi wanavyoelewa.
Kwa
upande wao wahitimu akiwemo Perpetua Msengi na John Martin, wamesema
wana matumaini makubwa ya kufaulu mtihihani huo, ingawa somo la hisabati
lilionekana kuwa gumu kwa upande wao.
Katika
hatua nyingine,Mkurugenzi Magayane amesema wamejipanga vizuri
kuhakikisha mwakani ufaulu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
katika wilaya hiyo mpya, unafikia aslimia 70.
“Hili linawezekana kwa sababu hivi sasa ufaulu wetu ni aslimia 51 wakati kitaifa unatakiwa uwe 31.
Kwa
hali hiyo nina imani kubwa kuwa lengo letu tutalifikia na ikiwezekana
tuvuke hilo lengo,ili mwaka 2015 tuweze kufikisha aslimia 80”, amesema
Magayane kwa kujiamini.
Post a Comment