KOCHA YANGA AFUTA KIKOSI CHA KWANZA, AFUTA VYEO




Kocha wa Yanga, Ernie Brandts ametamka kwamba mpaka sasa hajui nini kilichotokea katika kipindi cha pili, wakati Yanga ikitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Simba, lakini akawashukia mastaa katika kikosi hicho.


Brandts amesema ameshindwa kugundua kilichosababisha sare hiyo mpaka sasa, ambapo amewataka nyota katika kikosi hicho kutambua kuwa hakuna mtu mwenye nafasi ya kudumu ndani ya timu hiyo.

Brandts amesema katika mchezo uliopita dhidi ya Rhino Rangers ambao Yanga ilishinda kwa mabao 3-0, alikibadilisha kikosi hicho na kuwaweka nje baadhi ya wachezaji mastaa, ambapo amewataka wote katika timu yake kutambua kuwa timu yake ina jumla ya wachezaji 28 wenye uwezo mkubwa.

“Najiuliza kila mara nini kilitokea katika mchezo wetu dhidi ya Simba, nakosa jibu sahihi, lakini ndiyo soka, nimewaambia wachezaji wangu kuanzia mchezo wa jana (juzi), hakuna mtu mwenye namba ya kudumu, kila mtu ana haki sawa,” alisema Brandts.

“Nitampa nafasi mchezaji yeyote atakayekuwa sawa kwa asilimia mia moja, wachezaji wote wanatakiwa kutambua kuwa, timu yangu ina wachezaji 28, hakuna anayemzidi mwenzake kwa umuhimu.

“Sitaki kubadili kikosi mara kwa mara, lakini nitafanya hivyo kama nikigundua kuwa kuna wachezaji wameridhika na mafanikio ya muda mfupi,” alisisitiza

Post a Comment

Previous Post Next Post