Taarifa za watu mbalimbali kuhusu yaliyotukia huko Kilindi, Tanga

 

News Alert: Polisi wa kumwaga wapelekwa kilindi
by dionsio via JF

Idadi kubwa ya askari polisi FFU imepelekwa wilayani kilindi ili kuongeza nguvu kwa askali wenzao ambao inaonekana kuzidiwa nguvu na kundi lililofanya vurugu iliyosababisha kujeruhiwa kwa risasi OCD wa Kilindi.

Kundi hilo liliwasili hapa handeni majira ya saa 5 usiku, likitokea kibaha pwani, na lilikua linaongozwa na mkuu wa wilaya ya kibaha. Msafara huo ulipita kuonana na mkuu wa wilaya ya handeni ili kupata maelekezo toka kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa tanga, ambao walikutana hapa handeni kujadili hali tete ya handeni.

Kikao hicho kilidumu takribani masaa 5 tangia saa 9 hadi 1 ucku. Kikao hicho kilifanyika HILL TOWN HOTEL.
Picture
Askari majeruhi (picha kutoka kwa Assenga Oscar)

Endelea kusoma hapo chini, taarifa kama zilivyoripotiwa na watu mbalimbali kuhusu suala hili:
Ukweli kuhusu vurugu za kilindi
by Thegame via JF

Wakuu Jana nilikuwa Wilayani Kilindi kuna mashamba yangu nimenunua huko hivyo mara kwa mara huwa naenda. Mara nyingi nikiwa huko nimekuwa nikiambiwa na vibarua wangu kuwa kuna Jamaa wa Ansali Suna huwa wanafanyaga mazoezi makali ya kijeshi. wanasema wametoa taarifa mara nyingi kwa jeshi la polisi lakini bado hakuna ufuatiliaji wowote. Mimi kwa sababu nilikuwa na namba za mmoja wa maafisa usalama (usalama wa taifa) wilayani Handeni nikampigia simu na akakiri kuwa taarifa hizo wanazo ila kila mara kipira cha polisi kikienda huko Ansali suna wanakana kufanya mazoezi eti wao wanalima tu! Majibu hayo yalinishangaza mimi kwani sikutegemea hao jamaa wakihojiwa wangekubali kuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi. sasa jana nikiwa kwenye hicho kijiji wanakiita Kilwa Hao jamaa wa Ansali suna walikuwa wanataka kusafirisha Iliki kuja Dar. Kwa kawaida ukisafirisha mazao kutoka kijijini lazima ulipie ushuru wa kijiji na halmashauri. Jamaa walipoambiwa walipie ushuru wakagoma wakasema dini yao hairuhusu kulipa ushuru hiyo ni dhambi. hapo ndipo vurugu zilipoanzia! Wakamuua mwenyekiti wa hicho kijiji na kumjeruhi mwanakijiji mwingine kwa kumkata na panga tumboni. sasa vurugu ikawa ni hicho kikundi na wananchi wengine. Mimi nilipoona mambo yanazidi kuwa mabaya nikawasha gari nikatimua. njiani ndio nikakutana na askari polisi pamoja na huyo OCD ambaye nasikia nae wamemjeruhi! Ukweli ni kwamba hali ya kupuuzia mambo ya jeshi la polisi ndio imepelekea hadi hali kuwa mbaya kiasi hiki!

MKUU WA KITUO CHA POLISI CHA KILINDI EDWARD LUSEKELO APIGWA RISASI

Na Oscar Assenga, via assengaoscar blog, Kilindi — Askari wa Jeshi la Mgambo wa Kijiji cha Lwande Wilayani hapa, Salum Mgonje amekufa kwa kushambuliwa na mapanga na kundi la watuwaliokuwa wakipinga kitendo cha mwenzao kulipishwa ushuru wa manunuzi ya zao la hiliki wa Serikali ya Kijiji.

Mashambulizi hayo baadaye yalizusha mapigano baina ya kundi la watuwaliokuwa wakimsaidia mfanyabiashara huyo na askari wa jeshi la polisiwalipokwenda jioni kuwakamata waliohusika na mauaji ya mgambo.

Katika mapigano hayo, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kilindi Edward Lusekelo ambaye aliongoza askari waliokwenda kuwakamata waliohusika na mauaji ya Mgambo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi ya bunduki aina ya Short Gun.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamnada wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe ni kuwa askari wa mgambo aliuawa juzi mchana katika kijiji cha Lwande wakati mkuu wa kituo alijeruhiwa saa 2.30 jioni kijijini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa alisema chanzo cha mapiganohayo mfanyabiashara huyo kutoka Kijiji cha Lulago Kata ya Lwande kwenda Kijiji cha Lwande kununua hiliki ambapo baada ya kukaidi kulipa ushuru mgambo alilazimika kumtia msukosuko ili aweze kulipa kama ilivyo sheria ya kijiji.

“Ndipo zikatokea purukushani baina mgambo na wafanyabiashara ambapobaadaye walimshambulia kwa mapanga na kisha kumuua”alisema Liwowa.

Alisema taarifa za mauaji ya mgambo zilizpofika kituo cha Polisi ilimlazimu mkuu wa kituo kuongoza kikosi kilichokwenda kijiji cha Lwande kwa ajili ya kuwasaka waliohusika ndipo walipotokea likajitokeza kundi la watu wenye silaha wakaanza kuendesha mapigano naaskari wa jeshi la Polisi.

Akithibitisha habari hizi,Kamanda Massawe alisema tayari watu wannewanashikiliwa kuhusiana na tukio hili huku mkuu wa kituo cha Polisi akiwa amekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo kwa ajili matibabu.

Alisema mkuu huyo wa kituo amejeruhiwa mbavuni na mkononi ambapoinaonekana alifyatuliwa zaidi ya risasi tatu ambapo wengine waliojeruhiwa ni afisa mtendaji wa kata ya Lwande na askari mwingine wa Mgambo.


Tarehe 23/10/2013 (iliripotiwa) tukio la mkuu wa kituo cha polisi Songe wilayani Kilindi Insp. Lusekelo kupigwa risasi na kujeruhiwa na watu waliokuwa wakifanya mazoezi ya kivita.

Habari hiyo ilikosa sifa ya kuitwa habari ya kweli. 

Ukweli ni kuwa mkuu wa kituoa alikuwa amepigwa risasi na waislamu wa dhebebu la Sunn waliokuwa wakipinga ushuru wa mapato ya halmashauri.

Tarehe 21/10/2013 mfanyabiashara mmoja muislamu wa dhehebu la Sunn (wale wa ndevu na suruali fupi) aliyekuwa ananunua iliki ktk kijiji cha Lulago aligomea kulipa ushuru/kodi kwa halmashauri ya wilaya na kijiji kwa kuwa mambo ya kodi, ushuru na riba ni haramu kwa imani yao wao waislamu.

Ktk kutekeleza majukumu mtendaji wa kijiji akamtuma askari mgambo aende akamkamate yule bwana msunn ili achukuliwe hatua za kisheria. Hapo ndipo waislamu wale wa Sunn walipoamua kumtetea mwenzao (mfanyabiashara aliyegoma kulipa ushuru). Wakamkamata askari mgambo yule na kumuua kwa kumchinja.

Tarehe 23/10/2013 polisi waliwasili ktk kijiji hicho ili kushughulikia na kukamata wahalifu hao ambao ni waislamu walioua mgambo. Polisi hao waliongozwa na Insp. Lusekelo.

Polisi walipofika maeneo ambayo ni makazi ya waSUNN hao ndipo waislamu wale walimwahi Insp. Lusekelo kwa kumpiga risasi.

Hivyo maelezo (yaliyotokewa) kuwa mkuu wa kituo kapigwa risasi na watu waliokuwa wanafanya mazoezi ya kivita ni ukanjanja wa hali ya juu.

Kimsingi source ni waislamu wa "suruali fupi" waliotaka kujitangazia jamuhuri yao huru ya kiislamu kwani wamefanya matukio mengi kwa mwaka huu kama vile kuchoma kanisa la T.A.G moto, kuzuia waislamu wasio ansar Sunn kuswali msikitini kwao, kuzuia wakristu na waislamu wa kawaida kuteka maji ktk maeneo ambayo wao wamejitangazia jamuhuri yao ya SUNN, kuzuia biashara ya baa, kuzuia kupigwa kwa muziki wa aina yoyote kijiji chote nk. Kwa kutofanya hivyo unakamatwa na kupigwa sana na waislamu hao wenye imani kali.

Ukweli umefanyika uzembe wa serikali kwa kuacha kushughulikia matukio yote hayo hadi wakaota mapembe na kuwa na bunduki.

...

---
by Mcheza Karate

Post a Comment

Previous Post Next Post