Mejja Msanii mwenye vituko kutoka Kenya kuanza kufanya comedy hivi karibuni

mejja
Unapotazama video za msanii wa Genge maarufu kama Mejja kutoka Kenya, utagundua kwamba utamu wa muziki wake unapatikana zaidi katika video kuliko unaposikiliza kwenye radio peke yake, kwasababu amejaaliwa kipaji cha kuchekesha kuanzia unapomtazama sura yake tu yuko ki comedy sana.
Mejja ameamua kufuata ushauri wa mashabiki wake waliokuwa wakimshauri kuanza kufanya comedy sababu ameonekana kuwa comedian mzuri kupitia video za nyimbo zake zikiwemo Land Lord, Jana kuliendaje, Raundi hii si mchezo za nyingine alizoshirikishwa na Jua Cali.
Akizungumza katika mahojiano na Milele FM ya Kenya, Meme Hadhija aka Mejja ambaye yuko chini ya Calif Records amesema anakubali kuwa anakipaji cha kuchekesha na anatarajia kuanza kurekodi video za comedy na kuziweka youtube kwaajili ya mashabiki wake.
Tazama video ya wimbo wake ‘Landlord’ ucheke kidogo!


Post a Comment

Previous Post Next Post