Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya ‘Nakula Ujana’

nay-wa
Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa anatarajia kutoa wimbo mpya uitwao ‘Nakula Ujana’ ili kuwaonesha watu kuwa habahatishi.
Akizungumza jana, Nay alisema kumekuwa na mitazamo tofauti kutoka kwa watu kwamba yeye hubahatisha kwenye muziki na hivyo anataka kuwaonesha tofauti.
“Unajua nafanya muziki kwa uwezo wangu ndio maana tarehe 20 mwezi huu naachia wimbo mpya ambao kiukweli naamini utafanya vizuri. Muziki Gani watu walisema Diamond alisaidia ile ngoma kufanya poa,lakini kiukweli wimbo ulikuwa ni mzuri ndio maana ukafanya poa,” alisema Nay.
“Wimbo unaofuata utakuwa una ladha tofauti kwasababu kuna uimbaji wa tofauti ambao nimeufanya katika wimbo wangu ‘Nakula Ujana’ ili kupata ladha tofauti, ambayo naimani itafanya poa, na pia sipendi kukaa muda mrefu bila kufanya ngoma.”

Post a Comment

Previous Post Next Post