Umeshawahi kujikuta umekutana na msichana mrembo au mvulana
mtanashati, halafu siku ya pili ukakutana na pacha wake wanaofanana hadi
ukucha na ukaendeleza maongezi mlipoishia jana bila kugundua si yule wa
jana? Basi ndicho kilichomtokea Diamond Platnumz.
Coke Studio walimuandalia Platnumz ‘blind date’ ya mtoto wa kike
mrembo, ila bila yeye kujua kuwa wako wawili mapacha wanaofanana
(identical twins) na kumchezea mchezo. Baada ya kukutana na msichana wa
kwanza anayeitwa Rose, walizungumza kwa muda mfupi kisha mtoto huyo wa
Kikenya akaomba kwenda washroom. Huko alikuwa anasubiri pacha mwenzie
aitwaye Janet ambaye walibadilishana, aliyerudi kwa Diamond hakuwa yule
wa mwanzo.
Ila mwisho wa mchezo meneja wa Diamond alijifanya kumuita pembeni
kumuelekeza jambo, ndipo hapo walipojitokeza mapacha wote wawili na
kuketi pale pale alipokuwa Diamond, aliporudi akapigwa na butwaa asijue
ni yupi aliyeanza kuongea naye maana hata nguo walizovaa zinafanana.
Tazama video ufahamu ‘blind date’ iliishaje

إرسال تعليق