Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL
Group, Bi. Fatema Jaffer, akizungumza na waandishi wa habari juu ya
umuhimu wa kusaidia jamii kupitia (Corporate Social Responsibility) kama
njia mojawapo ya kupiga vita umaskini katika nchi za bara la Afrika. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu Ledger
Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni
ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi na Kushoto ni Irfaan Jaffer kutoka
MeTL.
.Lengo la maonyesho ni kusaka vipaji miongoni mwa vijana
.Kuanzia siku ya Krimasi hadi Boxing day zawadi mbalimbali na Tsh m kushindaniwa
Na Damas Makangale, MOblog
KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES
(MeTL) Tanzania kwa kushirikiana Ledger Plaza Bahari Beach wamezindua
maonyesho ya elimu ya mwaka kwa watoto nchini yenye kushindaniwa zawadi
mbalimbali na mshindi wa jumla kujinyakulia fedha taslimu Tsh5m.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Ledger Plaze Bahari Beach
Hotel, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Bi Fatema Jaffer, amesema kampuni
ya Metl ina jail maslahi ya wateja wake na watanzania kwa kupitia dhana
ya Kusaidia Jamii na Kujenga mahusiano (Corporate Social Responsibility)
kwa kusaidia kuinua vipaji vya watoto.
“Kwenye maonyesho haya ya wazi ya
kutazama vipaji mbalimbali vya watoto hasa kwenye elimu tumeamua
kudhamini maonyesho haya ili kusaidia jamii kuweza kukuza vipaji vyao
vya manufaa yao binafsi na jamii kwa ujumla,” amesema
Bi. Jaffer amesema kuwa katika
taifa la Tanzania kuna vipaji vingi hasa kwa vijana na watoto lakini
wanakosa msukumo na jamii kuwatia moyo ili vipaji vile viweze kufanya
kazi kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema maonyesho hayo yataanza rasmi kuanzia tarehe 25th,
26 na 27 kwenye viwanja vya Ledger Plaze Bahari Beach yenye dhumuni ya
kugundua, kutambua kuendeleza, kutia moyo na kupapanua vipaji vya watoto
vilivyojivicha kwenye jamii ya watanzania.
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo ya watoto na
vijana katika kuonyesha vipaji vyao mbalimbali.
Bi. Jaffer amesema maonyesho hayo yanaitwa (MO KIDS GOT TALENT)
kwa sababu mdhamini mkuu ni Metl na watakuwa tayari kufanya kazi bega
kwa began a watoto, vijana na wazazi wao katika kutambua, kuendeleza na
kukuza vipaji vya watoto kupitia maonyesho haya.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem
Souifi, amesema maonyesho hayo ni jukwaa pekee kwa vijana na watoto wa
Tanzania kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika elimu na Nyanja
nyingine za kuburudisha.
“Maonyesho haya yatawajenga vijana kuwa na ujasiri na kuzalisha
watu wenye mafanikio mbalimbali katika maisha na kusukuma gurudumu la
maendeleo mbele,” amesema
Amesema kuwa katika maonyesho hayo wazazi wanaombwa kuwaruhusu
watoto wao waende kwenye tamasha hilo kubwa na la kipekee kuandaliwa na
makapuni makubwa hapa nchini.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi,
akihamasisha wazazi nchini kuruhusu watoto wao wajitokeze kwa wingi siku
ya tarehe 25, 26 na 27 mwezi Desemba ambapo watoto 100 wa kwanza
kujisajili wataingia bure.
Kisura na
Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo akielezea umuhimu wa tamasha
hilo kubwa la Elimu kwa Vijana na manufaa ya kusaka vipaji kwenye umri
mdogo ambapo pia amewataka wazazi kuwapa ushirikiano wa kukuza vipaji
vya watoto wao.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer kwenye picha ya pamoja na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi pamoja na Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo.
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi, Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, Meneja Masoko Msaidizi wa
MeTL Group, Bw. Aunali Bandali, Irfaan Jaffer kutoka MeTL Group pamoja
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko.
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akimtembeza Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer maeneo mbalimbali ya hoteli hiyo.







إرسال تعليق