NADHANI ‘SCOLA’ INANIFUNGIA MWAKA VIZURI - AUNT EZEKIEL

AUNT EZEKIEL: NADHANI ‘SCOLA’ INANIFUNGIA MWAKA VIZURI.
Mara nyingi inapofika mwisho wa mwaka kila mtu walio wengi huangalia nini wamekifanya mwaka mzima na wapi pamebaki au kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Leo hapa anasimama msanii wa bongo movie maarufu kwa jina la Aunt Ezekieli ambaye ni muigizaji na muandaaji wa filamu za kibongo ambazo zinasambazwa na kampuni ya Steps intertainment hapa nchini na kutoa taswira ya kile alichokifanya kwenye uigizaji kwa mwaka huu hadi hapa alipofika.
“Namshukuru Mungu kwa kufika hadi hapa nilipofika kwa huu mwaka maana kuna wengi ambao walitamani tuwe nao leo lakini Mungu kawapenda zaidi. Kwa upande wa kutimiza yale niliyoyapanga kuyafanya kiuigizaji mwaka huu, naweza kusema kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa ijapokuwa kuna vitu vichache tu ambavyo bado na nadhani mwakani nitajipanga vizuri zaidi kweda na muda. Muvi nilizotoa ni nyingi but acha ‘Scola’ inifungie huu mwaka maana sidhani kama kuna muvi inatoka kwa mwaka huu tena yenye sura yangu na uzuri ndani ya Scola nimevaa uhusika vilivyo.” – Aunt Ezekiel

Post a Comment

Previous Post Next Post