Rais Kikwete awasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mazishi ya Nelson Mandela

 
Picture
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria. (picha hii na zilizopachikwa hapo chini ni kutoka Ikulu)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria usiku wa leo, Jumatatu, Desemba 9, 2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee  Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg.

Rais Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha mmoja wa
 viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.

Rais Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM.
Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Picture
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Picture
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana.

Post a Comment

أحدث أقدم