Ikiwa
ni siku ya tatu tangu kuachiwa kwa video ya Rapa toka kundi la Tip Top
Connection Madee video ya wimbo wa wimbo wake wa Tema Mate Tuwachape
baadhi ya maoni ya watu yamekua ni shaka juu ya video hiyo na kusema
kuwa ya kawaida kulingana na ilivyotegemewa kwa yeye kwenda kufanyia nje
ya nchi.
kama kawaida yetu tulimtafuta Madee na kumuuliza juu ya
hili suala,Madee anaanza kwa kusema>>‘Unajua huwezi kupata wote
wanaosifia na huwez kupata wote ambao wanachukia na kwenye vitabu vyetu
vya Quraan vinasema hauwezi ukapendwa na watu wote’
‘Ukipendwa na watu wote wewe una kasoro na ukichukiwa na watu wote
pia una kasoro kwa hiyo unatakiwa kubalance Kuna watu wengine wananambia
kitu Fulani na kitu Fulani hujakipatia umefata nini Kenya hao wapo na
kuna wengine wanasema yes mwanangu saivi kweli unaonyesha jinsi gani
umebadilika kama nyimbo yenyewe inavyosema,hivyo ni changamoto nafurahia
kuona watu wameangalia na kila mtu kasema chake’.
Hii ni video ya kwanza kwa Rapa Madee kwenda kufanya na Ogopa Video
ya Kenya,waweza kuitazama hapahapa,tumia sekunde kadhaa
kumsikiliza madee akielezea maoni ya watu alivyoyapokea.
Bonyeza play kusikiliza
إرسال تعليق