
SANTI
Cazorla amefunga mara mbili wakati Arsenal ikiifunga Fulham na kubaki
kwenye usukani wa Premier League, huku Manchester City nayo
ikiishindilia Cardiff 4-2 na kuandika rekodi ya kuvuka mabao 100 katika
mshindano yote msimu huu.

Fulham
waliwachanganya Gunners na kukaribia kufunga wakati shuti ya Steve
Sidwell ilipookolewa kabla Cazorla kufunga mara mbili dakika ya 57 na 62
kuipa ushindi Arsenal nyumbani Emirates.

Cazorla baada ya kutupia bao la kwanza

Cazorla akishangilia bao la pili

Wenger akiwapa dole wachezaji wake

Nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry alikuwepo uwanjani

Kipa wa Arsenal Szczesny akamzawadia shabiki jezi yake
Kwenye
dimba la Etihad, Edin Dzeko alifunga kwa shuti ya karibu kuipa City bao
la kuongoza dakika ya 14 likiwa la 100 katika mashindano yote msimu
huu, ingawa Cardiff ililalamika kama mpira kwanza ulishikwa na David
Silva.

Edin Dzeko akifunga moja kati ya mabao manne ya City

Navas naye akishangilia goli lake kiaina
Craig
Noone aliisawazishia Cardiff dakika ya 29, lakini Jesús Navas, Yaya
Toure na Sergio Aguero waliimarisha uongoz wa mechi kabla Fraizer
Campbell kuwafungia wageni bao la pili dakika mwisho.
Arsenal
iko mbele ya Manchester City kwa pointi moja na zimekuwa zikifukuzana
kwa kasi ya ajabu, ni wazi kuwa kuteleza kidogo tu kwa mmoja wao
kunaweza kumgharimu kula vumbi hadi mwishoni mwa msimu.
Post a Comment