SI mchezo, Ligi Kuu ya England mwaka huu ni shughuli pevu. Jumamosi,
Chelsea alikuwa kileleni, Jumapili, Manchester City na sasa ni Arsenal.
Kiasi cha pointi mbili tu kinazitenganisha timu tatu za juu.
Kikosi
cha Arsene Wenger kimerejea kileleni kufuatia ushindi wa mabao 2-1
ugenini usiku huu dhidi ya Aston Villa. Jack Wilshere alifunga dakika ya
34 na Olivier Giroud akafunga la pili dakika ya 35 Arsenal ikaongoza
2-0 kabla ya Cristian Benteke kuifungia Villa la kufutia machozi dakika
ya 76.
Arsenal
inarejea kileleni kwa pointi zake 48, ikiishusha Manchester City yenye
pointi 47 katika nafasi ya pili, mbele ya Chelsea yenye pointi 46.

إرسال تعليق