Beef Mpya ya Hiphop? Nash MC Vs Wakazi, chanzo ni picha ya Wakazi aliyopiga na KRS One

nash na wakaziInaonekana mwaka 2014 unaweza kukaribisha beef mpya ya hip hop Tanzania. Ni kati ya rapper wa ‘Tabia’ na ‘Naandika’ Nash MC dhidi ya Wakazi.
Issue ilianza baada ya Nash MC kuandika status Facebook kuponda picha ya Wakazi aliyopiga miaka mingi iliyopita na KRS One nchini Marekani na kuiweka kwenye ‘wall’ yake hivi karibuni. Katika status hiyo Nash alidai kuwa kupiga picha na KRS One hakumaanishi kuwa yeye (Wakazi) pia ni hip hop na kuhoji iwapo kama Shilole akipiga picha na rapper huyo mkongwe anaweza kujiita hip hop?
Akiongea na U Heard ya kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamis hii, Nash alisema kauli ile ilikuwa ya Facebook na iliishia pale.
“Mtandao haukunikutanisha na Wakazi, Wakazi nimekutana naye face 2 face,” alisema Nash. “Kwahiyo bado mshkaji, mimi navyoona kila kitu kiko sawa.”
Hata hivyo status hiyo ya Nash MC hajaichukuliwa kwa utani na Wakazi na kwamba tofauti na mawazo ya Nash kuwa ‘it’s all good’ rapper huyo wa ‘Touch’ aliandika status Facebook kumchana Nash kuwa kama anataka kukutana na KRS One au rappers aliopiga nao picha aseme na atapelekwa Marekani kutimiza ndoto yake.
“Sometimes mtu akisema kitu ambacho kinakugusa wewe vibaya njia ambayo na wewe unaweza kujibu ni kujibu kwa njia ambayo na yeye inaweza kumgusa vibaya,” Wakazi alimwambia Gossip Cop wa U Heard.
Wakazi amesema kauli ya Nash MC ni moja ya sababu muziki wa hip hop umeshuka Tanzania kwakuwa wasanii wanaendekeza malumbano yasiyo na tija.
Sikiliza zaidi hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post