Inaonekana mwaka 2014 unaweza kukaribisha beef mpya ya hip hop
Tanzania. Ni kati ya rapper wa ‘Tabia’ na ‘Naandika’ Nash MC dhidi ya
Wakazi.
Issue ilianza baada ya Nash MC kuandika status Facebook kuponda picha
ya Wakazi aliyopiga miaka mingi iliyopita na KRS One nchini Marekani na
kuiweka kwenye ‘wall’ yake hivi karibuni. Katika status hiyo Nash
alidai kuwa kupiga picha na KRS One hakumaanishi kuwa yeye (Wakazi) pia
ni hip hop na kuhoji iwapo kama Shilole akipiga picha na rapper huyo
mkongwe anaweza kujiita hip hop?
Akiongea na U Heard ya kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamis hii, Nash alisema kauli ile ilikuwa ya Facebook na iliishia pale.
“Mtandao haukunikutanisha na Wakazi, Wakazi nimekutana naye face 2
face,” alisema Nash. “Kwahiyo bado mshkaji, mimi navyoona kila kitu kiko
sawa.”
Hata hivyo status hiyo ya Nash MC hajaichukuliwa kwa utani na Wakazi
na kwamba tofauti na mawazo ya Nash kuwa ‘it’s all good’ rapper huyo wa
‘Touch’ aliandika status Facebook kumchana Nash kuwa kama anataka
kukutana na KRS One au rappers aliopiga nao picha aseme na atapelekwa
Marekani kutimiza ndoto yake.
“Sometimes mtu akisema kitu ambacho kinakugusa wewe vibaya njia
ambayo na wewe unaweza kujibu ni kujibu kwa njia ambayo na yeye inaweza
kumgusa vibaya,” Wakazi alimwambia Gossip Cop wa U Heard.
Wakazi amesema kauli ya Nash MC ni moja ya sababu muziki wa hip hop
umeshuka Tanzania kwakuwa wasanii wanaendekeza malumbano yasiyo na tija.
Sikiliza zaidi hapa.
إرسال تعليق