Madee amefunguka kwa mara ya kwanza kuwajibu watu wanaoikosoa
video ya wimbo wa Tema Tuwachape iliyofanywa na kampuni ya Ogop Videos
ya nchini Kenya kwa kusema hawezi kumridhisha kila mtu.
Madee ameiambia Bongo5 kuwa ni vigumu kwa mtu kufanya kitu kitakachopendwa na kila binadamu.
“Mimi kabla haijatoka na haijafika kwa wananchi, tulikuwa nayo kwenye
‘cabinet’ yetu. Tumeiona, tukaruhusu itoke,kwasababu hiyo ndio video
ambayo tulikuwa tunaitarajia,” amesema Madee. “Unajua huwezi kuwakataza
watu kuongea,kwasababu kila mtu ana chaguo lake. Unajua ninapoimba
nyimbo labda ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’ tayari kila mtu ana video yake
anayoitaka yeye kichwani, unakuta kila mtu ana mawazo yake kichwani.
Siwezi nikawafurahisha watu wote ambao wanataka video iwe hivi iwe hivi.
Nilichokifanya mimi, nimefanya video ambayo tunaipenda sisi kama Tip
Top Connection, ndio hiyo imetoka. Siwezi nikawafurahisha watu wote
kiukweli na wala siwezi kuwachukiza watu wote. Wapo ambao wanasema
wanaipenda na wapo ambao hawajaipenda. Ni kawaida huwezi kupendwa na
watu wote ni dhambi na huwezi chukiwa na watu wote,” alisisitiza Madee.
Nilichokifuata mimi kule ni mabadiliko ya video zangu. Nimefanya
video zangu nyingi tu Dar es salaam na kampuni za Tanzania. Nilikuwa
nataka mabadiliko ya muziki wangu, kwasababu natamani kufika mbele
ambako watu wengine wamefika ndio maana nikapanda ndege nikaenda Nairobi
kutafuta mabadiliko. Hayo ni kati ya mabadiliko ambayo nilikuwa
nayataka. Wale jamaa wana connection nzuri tu, connection yao unakuta
video zao nyingi zinachezwa katika television za kimataifa, kwahiyo
inakuwa rahisi na mimi kupenya kimataifa. Hayo ndio mabadiliko ambayo
nilikuwa nayataka mimi. So mtu akisema kwamba video hajaipenda huwezi
kuwafuraisha watu wote na wala syo suala la bei ambalo limefanya video
iwe hivyo. Sisi tulienda kushoot video suala bei tumelipa kama kawaida.
Mimi naona ninasonga mbele,”
Katika hatua nyingine, Madee amesema hivi karibuni anaelekea Nairobi
tena kuifuata kampuni ya Ogopa kushoot video ya remix ya ‘Pombe Yangu’
ambayo amewashirikisha P-Unit.
“Unajua nyimbo tayari ishafanya vizuri East Africa nzima, hata P-Unit
haikuwa kazi sana kuwashawishi kufanya hiyo ngoma. Aliyokuwa mstari wa
mbele sana kutaka hiyo kitu ifanyike alikuwa ni AY. Mimi nilimpa idea
AY, ‘bhana eeeh mimi nataka nifanye remix ya hii ngoma lakini sikuwa
nimewapoint P-Unit, nilimtaka Prezzo kwasababu ni msanii ambaye mimi
nilihisi atafit poa. Lakini AY yeye kama AY akasema ‘daah embu ngoja
tuangalie’. Baada ya siku kadhaa akanipigia simu akaniambia ‘bwana
P-Unit wanafanya’. AY akaorganize nao. Kwahiyo nimeanza kurecord ngoma
na video naenda Nairobi, Ogopa na baada ya kumalizika itatoka,” Madee
amefafanua.
“Matarajio yangu nataka kufanya vizuri East Africa mimi tayari
nimeshafanya vizuri Tanzania hakuna asiyemjua Madee Tanzania. Nataka
kufanya vizuri East Africa mzima ndio maana nikafanya na P-Unit ambao ni
wakubwa sana. Hawa jamaa wana tuzo mbili za Channel O, kwahiyo nikikaa
nao pamoja watu wasionijua watataka wanijue zaidi. Nina matumaini
nitafika mbali zaidi.”
إرسال تعليق