Jaguar aelezea mafanikio yake na kudai ‘ninafanya ‘clean business, siuzi dawa’

jaguar picMuimbaji wa Kenya, Jaguar amesema mali alizokuwa nazo zimetokana na juhudi zake katika muziki pamoja na biashara halali.
Jagua alikuwa akizungumza kwenye kipindi cha na Strictly Kenya cha East Africa Radio jana.
“Unajua nilifanya nyimbo mpya inaitwa ‘Kioo’ kitu cha kwanza kilinifanya nifanye huo wimbo yaani nikifungua Facebook watu wananiambia sijui ‘upo kilo ngapi’,mimi mwenyewe sijui hata madawa zinakaaje. I think yaani ni maombi mazuri,lakini mimi kwangu nafanya clean business yaani sifanyi vitu vya kichini chini, mimi siuzi dawa,” alisema.
“Unajua muziki kama mimi siwezi sema nafanya muziki full time kiukweli, lakini kwanza kitu cha kwanza, nimekuwa kwa game kama miaka 10,kwasababu watu wengine wanajua nimeanza juzi,lakini kama miaka 4. After kufanya miaka 4 niliona ‘eeeh bhana nafanya show zote zile pesa zinaisha’,that’s why nikaanza kujiinvest kidogo kidogo hivyo. Nilianza tu na movie shop,yaani ile ya kukodisha zile,yaani kidogo kidogo naanza taratibu business, naenda hivyo hivyo nafungua show room yangu ya magari,kidogo kidogo hivyo yaani ilinionyesha nilianza kutumia jina Jaguar kufika mbali,that’s why siku hizi unaniona na donate kutumia pesa zangu ni kwasababu nimepitia maisha hayo. Nimefukuzwa sana shule kwasababu ya karo ya shule. Ndio maana naamini hapa nilipofika ni watu walinifikisha. Kwahiyi kusaidia mtu sio kwasababu nauza dawa na mimi nilisaidiwa na watu mpaka kufika hapa,” aliongeza.
Akiongelea wimbo wake mpya, Kioo, Jaguar amesema alienda kwenye gereza la ukweli kuomba afanye video yake na alipokelewa kwa mikono miwili.
“Mimi sijionagi kama Jaguar kwasababu na believe binadamu wote tupo sawa,” alisema. “Siku ya kwanza naenda kuangalia maandalizi za jela ,walifurahia sana yaani ni kama napiga show, ‘Jaguar! Jaguar! wananiuliza wengi, walikuwa wanajua na mimi nimeshikwa kwasababu nimeingia tu,wanajua nimeingia tu ili niletewe uniform, nikawaambia ‘wazee nataka kushoot video hapa’ ,hawakuamini kwasababu wana,believe kuna klabu nzuri, nina magari mazuri. Nikawaambia ‘nataka kushoot video na nyinyi, kwasababu mimi naamini kila binadamu ana makosa’. Kwahiyo wale wako ndani sio kumaanisha wao ni watundu. Hakuna mtu hajawai fanya makosa. Kwahiyo nilitaka kuonyesha hakuna mtu hakuwahi fanya makosa, so nilikuwa nataka kuwaonyesha tupo pamoja na hata wakitoka wanaweza fanya kitu cha maana, kwasababu ukiangalia wameweza fanya kitu cha maana kama maactors na hakuna mtu tumeingia naye pale, wote wameshikwa.Kama sasa hivi nilikuwa na mwambia rais wetu,yaani vijana wako willing kufanya kazi,wakionyeshwa kama nikuact kama ni kuimba, mpaka nikaona nijitolee nitoe kadhaa.

Post a Comment

أحدث أقدم