![]() |
Wanajeshi wa Sudani Kusini waliporejesha mji wa Bor mikononi mwao, desemba 25 2013
RFI
|
Na RFI
Jeshi la Sudan Kusini limekua likiendesha kwa siku ya leo jumatatu
mapigano dhidi ya waasi wanomuunga mkono aliekua makamu wa rais, Rieka
Machar, ili kueweka katika himaya yake mji wa Bor, ambao unashikiliwa
kwa muda wa wiki kadhaa na waasi.
Hayo yanajiri wakati katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis-Ababa,
mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande mbili bado yanasuasua kuhusu
swala la kuwaachia huru wahungwa waliyokaribu na upinzani.
Mji wa Bor, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Jonglei (mashariki), bado uko
mikononi mwa waasi, lakini jeshi letu linaendelea na juhudi za
kuukomboa” Philip Aguer ameelezea AFP.
Tangu mapambano yaanze nchini Sudan kusini, mji wa mji mkuu wa jimbo la
Jonglei, umeshashikiliwa mara tatu na pande mbili tofauti (jeshi na
waasi), na kusababisha maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.
Philip Aguer, hata waasi, wanathibitisha kwamba mapigano yaliripotiwa
kati ya pande mbili jana jumapili alaasiri katika eneo linalopatikana
kwenye umbali wa kilomita ishirini na mji wa Juba.
“Mapigano yalianza saa kumi (...) wakati (rais wa Sudan Kusini) Salva
Kiir alituma idadi kubwa ya wanajeshi kwa kushambulia ngome zetu”,
wamefahamisha waasi katika tangazo ambalo wametoa mjni Addis-Ababa,
ambako kunafanyika mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya
Sudan Kusini na waasi wanaomuunga mkono Riek Machar.
“ Gari liliokua linasafirisha wanajeshi lilichomwa moto, wakati ambapo
mapigano hayo yalidumu saa mbili”, limeongeza tangazo hilo.
Philip Aguer, kwa upande wake, amefahamisha kwamba ni shambulio lililoendeshwa na wanajeshi wasiounga mkono serikali.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano hayo yanaendelea kuathiri taifa
hilo changa, tangu desemba 15 kutokana na kutoelewana kati ya rais
Salva Kiir na makamu wa wake, Riek Machar, ambae aliamuachisha kazi
katika mwezi wa julai mwaka jana. Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi
ya 1,000 kupoteza maisha na takribani 400,000 kuyahama makaazi yao.
Katika kitongoji cha Minkamman, kinachopatikana karibu kilomita 25
kusini magharibi mwa mji wa Bor, kuna wakimbizi wengi wa ndani, ambako
zaidi ya watu 80,000 wanapewa hifadhi, huku watu 50,000 wakiwa
wamekimbilia nchi jirani.
Salva Kiir aliwatuhumu wapinzani wake jaribio la mapinduzi, huku Riek Machar akikanusha madai hayo.
Hata hivo, mazungumzo yanaendelea, licha yakua bado yanasuasua kutokana
na kwamba yanakabiliwa na pingamizi ya kusitisha mapigano kabla ya
kuachiwa huru kwa wanasiasa waliyo karibu na Riek Machar, ambao
wanaziwiliwa jela.
Waasi wanaomba kuachiwa huru kwa wanasiasa hao ili washiriki moja kwa
moja katika mazungumzo, lakini serikali ya Juba inakataa, ikibaini
kwamba lazima wahukumiwe.
Pande hizo mbili husika katika mgogoro wa Sudan Kusini wamekutana leo jumatatu kwa mazungumzo.
“Mazungumzo haya tunataraji kua yatazaa matunda na kusitisha mapigano,
iwapo hakutatokea mambo mengine”, ameelezea AFP, kiongozi wa ujumbe wa
serikali, Michael Makuei.
Ujumbe wa waasi haukutoa tangazo lolote.
Mwishoni mwa juma, wasuluhishi kutoka Afrika mashariki wakishirikiana na
mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya Sudan Kusini, Donald
Booth, walikutana kwa mazungumzo na Riek Machar katika sehemu ilosiri
nchini Sudan Kusini.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr

إرسال تعليق