Lady Jaydee Akanusha Kuwa Mchoyo Wa Collaboration Na Wasanii Wengine…

JAY DEE
Takribani masaa manne sasa, tangu malkia wa Bongo fleva Tanzania, Lady Jaydee ashushe orodha ndefu ya nyimbo ambazo amefanikiwa kufanya na wasanii wengine, kwa maana ya kushirikishwa (collaboration) kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook mapema leo.
Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya marafiki ambao wameshiriki kwenye kutoa maoni yao, baadhi yao wameonekana kukubaliana na hilo lakini kwa upande mwingine baadhi wamehoji kwanini hajashirikiana na baadhi yao..
JIDE ORIGINAL
JIDE ORIGINAL  2
Ni orodha ndefu ambayo Jide amewathibitishia wapenzi wa burudani kuwa yeye si mchoyo wa collabo, na si nyimbo hizo tu bali anaamini kuna baadhi amezisahau. Kiasi kikubwa cha wapenzi wa burudani walifurahia orodha hiyo na kuendelea kumtia moyo wa kuendelea mbele na juhudi zaidi na kuwasaidia wengine
JIDE7
Hata hivyo, mashabiki na wapenzi hao wa burudani walihoji kwanini katika nyimbo zote hizo alizoorodhesha, hits zote alizozifanya na Hamis Mwinjuma, famously known as Mwana FA zimetengwa, kunani? Hits  kama “Alikufa Kwa Ngoma”, “Msiache kuongea”, “Hawajui” zote zilitamba kwenye chati kadhaa za muziki
Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Jide walihoji,
JIDE 6
JIDE 2
JIDE3


Post a Comment

Previous Post Next Post