Mh. Lowassa aongoza harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala,jijini Dar

 
Brass Band ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya Harambee ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya Mbagala,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo ambayo iliambatana na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zilipatikana kwenye harambee hiyo.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipiga vyombo mbali mbali vya Muziki kwenye Matembezo hayo.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) ambaye ndie aliekuwa Mgeni Rasmi kwenye harambee hiyo akionekana kwenda sambamba na Matembezi hayo.
Mh. Lowassa akiwasalimia Wanafunzi,Walimu na Wazazi wa Watoto wanaosoma katika Shule mbali mbali za Sekondari eneo la Mbagara jijini Dar es Salaam leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post