
Brass Band ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya Harambee
ya Kuchangisha fedha za Ujenzi wa Shule za Sekondani za Kata katika Tarafa ya
Mbagala,iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mt. Anthony,Mbabala
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo ambayo
iliambatana na Uzinduzi wa Mahafali ya Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Nne
alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa.ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zilipatikana kwenye harambee
hiyo.



Baadhi ya Askari wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipiga vyombo mbali mbali vya Muziki kwenye
Matembezo hayo.

Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) ambaye ndie aliekuwa
Mgeni Rasmi kwenye harambee hiyo akionekana kwenda sambamba na Matembezi
hayo.

Mh. Lowassa akiwasalimia
Wanafunzi,Walimu na Wazazi wa Watoto wanaosoma katika Shule mbali mbali za
Sekondari eneo la Mbagara jijini Dar es Salaam leo.
إرسال تعليق