Mwandishi Fortunata azikwa kijijini kwao Mdawi


MAMIA ya wakazi wa kijiji cha Mdawi,kata ya Kimochi wilayani Moshi vijijini,jana waliuhifadhi katika nyumba ya milele,mwili wa aliyekuwa mwandishi wa gazeti la HABARILEO mkoani Manyara, Marehemu Fortunata Ringo(29).


Wanahabari wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Fortunata, tayari
kwa ajili ya maziko kijijini kwao  Mdawi kata ya Kimochi.


Miongoni mwa waombolezaji ni pamoja na mwandishi mwandamizi na mwakilishi wa Kampuni ya Tanzania standard Newspapers (TSN) mkoani Kilimanjaro,Deus Ngowi ambaye alisema marehemu alikuwa mchapakazi.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari katika mikoa ya Arusha,Manyara na Klabu ya wanahabari mkoani Kilimanjaro(MECKI).

Katika ibada ya mazishi iliyoendeshwa na mchungaji,Elizabeth Masue wa Kanisa La kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) usharika wa usharika wa Mowaleni Komfuru,alitaka waumini kumkumbuka Mungu.

Alisema kwa sasa baadhi ya waumini wametekwa na anasa za dunia na badala yake wamekosa muda wa kumtumikia Mungu jambo ambalo linapaswa kubadilishwa ili kufuata maandiko matakatifu.

“Mungu amependa tukutane katika mazishi haya ya mpendwa wetu Fortunata ili kukumbushana maagizo yake….tumekuwa busy kutafuta fedha,kila kukicha ni fedha,tumemsahau Mungu, tumrudie” alisema.

Alisema maisha ya duniani ni mafupi mno na kwamba inawalazimu waumini kumrejea Mungu na kutenda yale aliyoagiza katika Biblia ambayo ndiyo ukombizi uliobaki.

Mchungaji Masue alisema ni wakati muafaka kwa waumini kutafakari wapo wapi na wanaelekea wapi kwani kwa kufanya mambo ya kumchukiza Mungu ni kulinyima taifa Baraka.

Fortunate alifariki Jan 10 jijini Dar baada ya kuugua maradhi ya kupungukiwa damu aliyopata mwaka 2011.

Post a Comment

Previous Post Next Post