MAMIA ya wakazi wa kijiji
cha Mdawi,kata ya Kimochi wilayani Moshi vijijini,jana
waliuhifadhi katika nyumba ya milele,mwili wa aliyekuwa mwandishi wa gazeti la
HABARILEO mkoani Manyara, Marehemu Fortunata Ringo(29).
|
Wanahabari
wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Fortunata, tayari
kwa
ajili ya maziko kijijini kwao Mdawi kata
ya Kimochi.
|
Miongoni mwa waombolezaji
ni pamoja na mwandishi mwandamizi na mwakilishi wa Kampuni ya
Tanzania standard Newspapers (TSN) mkoani Kilimanjaro,Deus Ngowi
ambaye alisema marehemu alikuwa mchapakazi.
Mazishi hayo pia
yalihudhuriwa na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari katika mikoa ya
Arusha,Manyara na Klabu ya wanahabari mkoani Kilimanjaro(MECKI).
Katika ibada ya mazishi
iliyoendeshwa na mchungaji,Elizabeth Masue wa Kanisa La kiinjili la
Kilutheri Tanzania(KKKT) usharika wa usharika wa Mowaleni Komfuru,alitaka
waumini kumkumbuka Mungu.
Alisema kwa sasa baadhi
ya waumini wametekwa na anasa za dunia na badala yake wamekosa muda
wa kumtumikia Mungu jambo ambalo linapaswa kubadilishwa ili kufuata
maandiko matakatifu.
“Mungu amependa tukutane
katika mazishi haya ya mpendwa wetu Fortunata ili kukumbushana maagizo
yake….tumekuwa busy kutafuta fedha,kila kukicha ni
fedha,tumemsahau Mungu, tumrudie” alisema.
Alisema maisha ya duniani
ni mafupi mno na kwamba inawalazimu waumini kumrejea Mungu na kutenda
yale aliyoagiza katika Biblia ambayo ndiyo ukombizi uliobaki.
Mchungaji Masue alisema
ni wakati muafaka kwa waumini kutafakari wapo wapi na wanaelekea wapi
kwani kwa kufanya mambo ya kumchukiza Mungu ni kulinyima taifa Baraka.
Fortunate alifariki Jan
10 jijini Dar baada ya kuugua maradhi ya kupungukiwa damu
aliyopata mwaka 2011.
إرسال تعليق