
Baadhi ya taarifa zilizofichuliwa na Edward Snowden
Rais Wa Marekani Barrack Obama
amekiagiza kitengo cha ujasusi nchini humo kusitisha ukusanyaji wa
habari kutoka kwa simu za mamilioni ya raia nchini humo na hata katika
mataifa ya kigeni.
Akizungumza mjini Washington Obama pia
amewaahidi viongozi wa nchi washirika wa Marekani kwamba taifa lake
halitachunguza mawasiliano yao ya faragha hadi itakapolazimika kufanya
hivyo kutokana na maswala ya ki-usalama.Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa makundi ya wanaharakati watashangazwa na hatua ya kitengo hicho kuendelea kumiliki habari nyingi za simu walizokusanya na kwamba haijulikana watazifanyia nini habari hizo.
Hadhi ya kitengo cha ujasusi nchini marekani imeshushwa na ufichuzi wa bwana Snowden.
Wakati huohuo hotuba ya rais Obama kuhusu mabadiliko ya mpango wa upelelezi wa marekani yamepongezwa nchini Ujerumani.
Uhusiano kati ya Berlin na Washington uliwekwa katika mizani mwaka uliopita baada ya kubainika kwamba marekani ilidukua simu ya chansela wa Ujerumani Angela Merkel.
- BBC
إرسال تعليق