Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa
Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa
matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet kunawatenga watu
kutoka kwa familia na marafiki zao.
Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali.
“Internet… inatoa nafasi ya mafanikio mengi. “Hiki ni kitu kizuri bila
shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema Papa.
Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa
amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio
nyaya tupu.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu
kukutana na kujuliana hali,huku akiwataka waumini wa kikatoliki
kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati
wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
Papa ana akaunti kwenye mitandao ya Twitter na Facebook ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni wengi.
Source:BBC
Post a Comment