
MANCHESTER
United imetangaza rasmi kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya
pauni milioni 37.1 mara baada ya kufuzu vipimo vya afya siku ya
Jumamosi.
Kiungo huyo wa Hispania aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United (Carrington) kwa helkopta mapema Jumamosi kabla ya kwenda kufanya vipimo vya afya.
Baadae
United ikatupia picha ikimuonyesha Mata akiwa ametinga fulana ya klabu
sambamba na kocha David Moyes wakati wa kusani mkataba.
Mata sasa anaweza kucheza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumanne dhidi ya Cardiff City.
إرسال تعليق