MZAHA
na uzembe unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wilayani Kiteto na
mkoani Manyara katika kusuluhisha mgogoro wa wafugaji na wakulima,
umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 13 usiku wa kuamkia jana.
Mbali
ya vifo hivyo, vita hiyo iliyaonza majira ya saa 11 alfajiri kwa
kutumia silaha za moto na jadi, imesababisha majeruhi zaidi ya 50 huku
wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Baadhi
ya wakulima waliozungumza na mwandishi wa habari hizi jana, walisema
wafugaji wa jamii ya Kimasai walivamia nyumba zao alfajiri ya kuamkia
jana na kuzichoma moto, huku wakitoa kipigo kwa kila mtu waliyemuona
mbele yao.
Habari
hizo zinasema wakulima waliokuwa wabishi na kujaribu kupambana na kundi
hilo la wafugaji wa Kimasai, walipigwa risasi na kupoteza maisha.
Hali
ya baadhi ya vijiji wilaya Kiteto ilionekana kama uwanja wa vita kwani
milio ya risasi na milipuko ya moto ilisikika kila kona.
Kuona
hivyo, baadhi ya familia hasa wanawake na watoto, walilazimika
kukimbilia porini ambako wafugaji hao waliwafuata na kuwaua.
Taarifa
za awali zilizotolewa na wakulima zilisema kuwa mapigano hayo sasa
yameingia katika hatua mbaya kwani kuna kundi kubwa la jamii ya wafugaji
wa Kimasai wakiwa na silaha za kivita.
Mmoja wa wakulima, Machite, alisema eneo la Laitimi lenye wakulima wengi, ndilo lililoathirika zaidi na mapigano hayo.
“Sasa
ngogoro huu unazidi kukua na unazidi kutumaliza sana na hiyo
inasabaishwa na viongozi kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji kwa madai
kuwa watawafukuza wakulima ili Wamasai wachunge mifugo yao.
“Juzi
tulifanya mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo juu ya
kutatua migogoro na mfugaji mmoja wa Kimasai alieleza kuwa kiongozi
mmoja wilayani Kiteto anachangisha fedha kwa ajili ya kuwapa maeneo ya
kuchungia,” alisema.
Akizungumzia
mgogoro huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema tangu kuanza kwa
mapigano hadi sasa watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Mkilamali Mpwapwa, alisema idadi ya
waliofariki ambao miili yao imeshapatikana ni sita, lakini kuna
uwezekano wa kuwapo wengine porini, hivyo wanaendelea kuwatafuta.
Kamanda huyo alisema bado wanafanya tathimini kujua idadi ya nyumba zilizochomwa na hasara iliyopatikana.
Alisema jeshi lake limeimarisha ulinzi na linawasaka wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo.
Source: Tanzania Daima










إرسال تعليق