Upinzani nchini Ukraine umeapa kuendelea na maandamano


Upinzani nchini Ukraine umetoa saa ishirini na nne kwa utawala wa nchi hiyo kuitisha uchaguzi mkuu, ama nchi hiyo ijiandae kwa maandamano makubwa zaidi.



Tangazo la upinzani limetolewa wakati huu kukiripotiwa maandamano zaidi mjini Kiev ambapo watu watano wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia.

Hapo jana serikali ya nchi hio ilianza utekelezaji wa sheria yake inayokataza maandamano kwenye sehemu za umma sheria ambayo imewafanya waandamanaji kuwa wagumu zaidi kuondoka kwenye maeneo ambayo wanayakalia kwa sasa.

Waziri mkuu wa taifa hilo, amesisitiza kuwa kile kinanchofanywa na upinzani kinaenda kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ingawa amekiri kuwa serikali yake huenda ikatekeleza matakwa ya upinzani kuitisha uchaguzi mwingine.

Rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch aliwatolea wito wananchi wake jana kutoshirikiana na wabaguzi wanaochochea machafuko katika mji mkuu wa taifa hilo wa Kiev yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya wanne.

Post a Comment

أحدث أقدم