Kikosi cha Twiga Stars kinashuka Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia leo kuwavaa wenyeji Zambia (Shepolopolo) katika
mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayooneshwa
moja moja ‘live’ na televisheni ya Shirika la Taifa la Utangazaji la
Zambia (ZNBC).
Mechi
hiyo itaanza saa 9 kamili mchana kwa saa za Zambia ambapo Tanzania
itakuwa saa 10 kamili jioni huku Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian
Kaijage akiwa tayari ametangaza ‘silaha’ zake kwa mechi hiyo ya kwanza
ya raundi ya kwanza.
Watakaoanza
kupeperusha bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambayo kiingilio ni
bure kwa majukwaa yote isipokuwa lile kuu ni; Fatuma Omari 1, Fatuma
Bashiru 17, Donisia Daniel 2, Fatuma Issa 5, Evelyn Sekikubo 15, Sophia
Mwasikili 16, Vumilia Maarifa 10, Mwapewa Mtumwa 9, Asha Rashid 14, Etoe
Mlenzi 13 na Shelida Boniface 7.
Wachezaji
wa akiba ni Maimuna Said 18, Fatuma Hassan 12, Zena Khamis 6, Esther
Chabruma 8, Amina Ally 4, Therese Yona 11 na Happiness Hezron 3.
إرسال تعليق