| Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga. |
Na Sweetbert Lukonge Via GPL KWELI
biashara ni matangazo, siku chache baada ya kuonyesha uwezo mzuri kwenye
mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri,
imefahamika kuwa ule mpango wa timu hiyo ya Misri kuwasajili Nadir
Haruob ‘Canavaro’ na Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga, umeendelea kwa
kasi.
Habari za uhakika ni kuwa Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi
ya Mabingwa, wametuma mashushushu wake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kufuatilia nyendo za wachezaji hao kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho
ya kuwasajili.
Al Ahly ilivutiwa na wachezaji hao kutokana na uwezo mzuri katika mechi zote mbili, ile ya Dar na ile ya Alexandria, Misri, ambapo Yanga iliondolewa kwa penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1.
Al Ahly ilivutiwa na wachezaji hao kutokana na uwezo mzuri katika mechi zote mbili, ile ya Dar na ile ya Alexandria, Misri, ambapo Yanga iliondolewa kwa penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1.
Habari ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya Yanga zimesema
kuwa Waarabu hao wametua jijini Dar es Salaam, juzi Alhamisi na leo
Jumamosi wataenda Morogoro kwa lengo la kuwafuatilia nyota hao katika
mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri.
“Tulijua ni utani kumbe jamaa wapo siriasi, mashushushu wao wametua
nchini jana (juzi) na kesho (leo) wataenda Morogoro kuwashuhudia
wachezaji hao watakapokuwa wanacheza dhidi ya Mtibwa.
Nadir Haruob ‘Canavaro’.
“Hata hivyo, mara baada ya kufika nchini waliwasiliana na mmoja wa
viongozi wetu na kumwambia kuwa watakuwa hapa kwa zaidi ya wiki mbili
wakiwafuatilia wachezaji hao,” alisema mtoa habari huyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alipoulizwa juu ya suala hilo
hakuwa tayari kulizungumzia, alisema: “Siwezi kulizungumzia suala hilo,
nipo bize sana, nitakuwa nikifanya kazi ya msemaji ambaye hatanilipa.”
Hata hivyo, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alipoulizwa juu ya suala hilo alisema: “Sina taarifa yoyote juu ya watu hao.”
Tangu ujio wa kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, katikati ya msimu
huu, Dida amekuwa chaguo la kwanza wakati Cannavaro naye amerejea katika
kiwango cha juu baada ya kupata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa
timu yake waliokuwa wakimshutumu kushuka kiwango.

Post a Comment