ALICHOKISEMA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA JIMBO LA CHALINZE BAADA YA KUWEKEWA PINGAMIZI

.Jana March 13 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ilitoka stori iliyowahusisha Wagombea Ubunge jimbo la Chalinze ambao ni Fabian Leonard Skauki wa CUF na Matheo wa  Chadema juu ya kusemekana kuwa Mathayo Mang’unda Torongey aliongopa kwenye ujazaji wa fomu zake za kugombea Ubunge jimbo hilo.

Leo millardayo.com imefika tena hadi Bagamoyo makao makuu ya wilaya Chadema kwa ajili ya kufahamu undani wa madai hayo ya Mgombea wa Cuf ambapo Matheo ameanza kwa kusema>>’kwanza labda niweke sawa zile fomu hakuna sehemu ambayo inasema uambatanishe na vielelezo vya shughuli unayofanya’
MATHEO
‘Kiuhalisia mimi ni mfanyabiashara wa siku nyingi nafanya biashara na maduka ya nyama kuhusu kughushi sahihi ya wadhamini hili ni suala ambalo sio la ukweli kwa sababu wakati  tunarudisha fomu ilihakikiwa na mkurugenzi ambae ndiye msimamizi wa uchaguzi’
‘Na sio saini za mkono peke yake zipo za dole gumba na zipo mchanganyiko na tunazo pia zile shahada za wapiga kura,tulifanya uhakiki na shahada zenyewe hivyo mkurugenzi alihakiki na kusema zipo sawa sawa’

‘Kuhusu kusema kuwa mimi sio Mtanzania hilo suala sio la kwangu nafikiri la uhamiaji au wanalo wenyewe lakini mimi ni Mtanzania halalai na ninacho kitambulisho cha kupigia kura ambacho nafikiri watanzania wengi wanakitumia’
CHANZO:MILLARDAYO.COM

Post a Comment

أحدث أقدم