Mwenyekiti wa Benki ya Covenant
Balozi Salome Sijaona
akimkabidhi mratibu wa
uhamasishaji wa vikundi vya Wilaya ya Temeke Bi.Tukae Kondo ufunguo wa pikipiki
baada ya kuwapatia mikopo wajasiliamali mbalimbali.Benki hiyo kwa kushirikiana
na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi imewawezesha wajasiriamali
wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo na mitaji. Hafla hiyo imefanyika makao makuu
ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat
bank Sabetha Mwambenja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenat Sabetha Mwambenja, akiwasisitizia jambo juu
ya kurejesha mikopo baadhi ya wajasiriamali waliopata mikopo ya pikipiki iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na
umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasilia mali
wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo . Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki
hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa bodi wa benki
hiyo Balozi Salome Sijaona
Mwenyekiti wa Benki ya Covenant
Balozi Salome Sijaona
akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi
cha Mshikamano cha Yombo Vituka cha
jijini Dar es Salaam,Charles Rweyemamu
ufunguo wa gari aina ya basi lenye thamani ya shilingi Milioni 45 .Benki
hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha
wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo. Hafla hiyo imefanyika makao
makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Covenat bank Sabetha Mwambenja.
*********
Benki ya
Covenant kwa kushirikiana na Umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi
katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini wamewawezeha wajasiriamali zaidi
ya 60 kujikwamua kimaisha kwa kuwapatia mikopo ya mitaji ambayo imejumuisha,
Basi za abiria, Pikipiki za miguu mitatu maarufu kama bajaji pamoja na pikipiki
Ushirikiano utakaowezesha zaidi ya wajasiriamali wadogo takribani milioni 6.8
ambao wote ni wanachama wa chama hicho nchini.
Akizunumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Balozi.Salome Sijaona amesema kuwa
benki yake imeendelea kuwapa kipaumbele watu wote wa chini ambao hawajafikiwa
na huduma za kibenki na sasa wamewekeza zaidi katika kuwawezesha wajasiriamali
hao kwa kuwapatia mitaji endelevu itakayo wawezesha kuingiza kuwaingizia kipato
moja kwa moja.
“Benki yetu iko katika msitari wa mbele kuwawezesha Watanzania na wajasiriamali ambao hawako katika sekta rasmi na hawajafikiwa na huduma za kibenki, katika kuhakikisha tunafikia malengo haya, tumeweza kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha tunafikisha huduma zetu kwa watu wote,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa.
Post a Comment