“PRESS RELEASE” TAREHE 18.03.2014
- MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
- MAHABUSU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJARIBU KUJINYONGA KWA KUTUMIA SHATI LAKE.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
- GARI AINA YA NOAH [IT] YAIBWA HUKO WILAYANI MOMBA – TUNDUMA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MFANYABIASHARA MMOJA AKIWA ANAMILIKIA SILAHA KINYUME CHA SHERIA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KYELA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MNAZI
ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MTO RUAHA. TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA
KITONGOJI CHA IGUNULA, KIJIJI CHA MNAZI, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA
MBARALI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA UCHAWI. MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA INNOCENT NKWANDA (24) MKAZI WA WILAYA YA MBOZI
AMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MAHABUSU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJARIBU KUJINYONGA KWA KUTUMIA SHATI LAKE.
MAHABUSU
MMOJA AITWAYE NASSON PAULO [70] MKAZI WA RUIWA WILAYANI MBARALI MKOANI
MBEYA ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUJINYONGA AKIWA MAHABUSU KATIKA
KITUO CHA POLISI KATI MBEYA MNAMO TAREHE 17/03/2014 MAJIRA YA SAA 04:50
ALFAJIRI KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAUAJI.
MAREHEMU
HUYO ALIKAMATWA KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAUAJI INAYODAIWA KUYAFANYA
TAREHE 12.02.2014 KWA KUMUUA KWA KUMPIGA NYUNDO KICHWANI DONALD JOSEPH@
YUSUPH ALIYEDAIWA KUMUIBIA NG’OMBE WAKE NA KISHA KUFICHA MABAKI YA
MWILI WAKE KUSIKOJULIKANA.
MAREHEMU
NASSON PAULO ALIKAMATWA BAADA YA KUPATIKANA KWA USHAHIDI TOKA KWA WATU
WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO LA MAUAJI NA ALIPOHOJIWA ALIAHIDI KWA
WAPELELEZI KUWA SIKU INAYOFUATA YAANI TAREHE 17.03.2014 ATAKWENDA
KUONYESHA ENEO ALIPOPELEKA MWILI HUO. MTUHUMIWA ALIRUDISHWA MAHABUSU.
MNAMO
MAJIRA YA SAA 04.50 ALFAJIRI WAKATI MTUHUMIWA AKIWA MAHABUSU CHUMBA
CHA PEKEE YAKE KUTOKANA NA UMRI WAKE NDIPO ALIFANYA JARIBIO LA
KUJINYONGA KWA KTUMIA SHATI YAKE. HATA HIVYO ASKARI WA ZAMU WALIFIKA NA
KUMKUTA CHINI AKIPUMUA KWA SHIDA HALI ILIYOWAFANYA WAMKIMBIZE HOSPITALI
YA RUFAA KWA MATIBABU YA HARAKA LAKINI HAKUWEZA KUCHUKUA MUDA MREFU NA
HATIMAYE ALIFARIKI DUNIA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL MWASUNDA (39) MFANYABIASHARA,
MKAZI WA MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA
KUACHA NJIA NA KUPINDUKA. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 17.03.2014
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI KATIKA KIJIJI CHA ISALALO, KATA NA TARAFA
YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI BARABARA YA MLOWO/MSANGANO BAADA YA GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.634 CTN AINA YA MITSUBISHI FUSO TIPPER
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE
KUACHA NJIA NA KUPINDUKA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
GARI AINA YA NOAH [IT] YAIBWA HUKO WILAYANI MOMBA – TUNDUMA.
GARI
LENYE NAMBA IT 1163 AINA YA TOYOTA NOAH RANGI NYEUPE ILIYOKUWA
IKISAFIRISHWA NA KAMPUNI YA TRIPPLE D KWENDA NCHINI ZAMBIA AMEIBWA USIKU
WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 HUKO KATIKA MTAA WA SOGEA – TUNDUMA,
KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA. GARI HIYO ILIIBWA WAKATI
IKIWA IMEEGESHWA KATIKA BAR IITWAYO MSASANI BAADA YA WATU HAO KUMVAMIA
MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA BENSON SIMUMBA (56) MLINZI KAMPUNI YA PANIC
SYSTEM GROUP NA KISHA KUMFUNGA KAMBA NA KUIBA GARI HILO. AIDHA WATU HAO
WALIMJERUHI KWA KUMKATA MAPANGA KWENYE PAJI LA USO NA KISOGONI HAMIS
MLONDWE YANDA (31) MKUSANYA USHURU WA ENEO HILO, MKAZI WA MTAA WA MWAKA
-TUNDUMA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MFANYABIASHARA MMOJA AKIWA ANAMILIKIA SILAHA KINYUME CHA SHERIA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MFANYABIASHARA MMOJA AITWAYE
MAULID JULIUS MWANGILA (43) MKAZI WA MTAA WA MWAKA-UWANJANI TUNDUMA
AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA MOJA AINA YA BASTOLA ILIYOTENGENEZWA
KIENYEJI INAYOTUMIA RISASI ZA S/GUN. MTUHUMIWA ALIKAMATWA TAREHE
17.03.2014 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU KATIKA MTAA WA MWAKA- UWANJANI –
TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA KATIKA MSAKO
ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. UPELELEZI UNAENDELEA NA UTAKAPO KAMILIKA
NA KUTHIBITIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE
TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUMILIKI SILAHA, VINGINEVYO WASALIMISHE WENYEWE
SILAHA HIZO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KYELA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTU
MMOJA AITWAYE BARAKA ADAM (27) MKAZI WA KYELA KATI ANASHIKILIWA NA JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI AINA YA BWANA GIN KATONI 27 KUTOKA NCHINI MALAWI. MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI KATIKA
MTAA WA KYELA MJINI, KATA YA KYELA –KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA KATIKA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BIDHAA
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KAMWE
JESHI LA POLISI HALITASITA KUMKAMATA NA KAMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA
MTU YEYOTE ATAKAYE BAINIKA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HIYO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment