Rapper Black wa Uswazi amesema hawezi kugombana na Adam Juma na anapenda video yake ya ‘Kilonya’ afanye naye iwapo akikubali.
Rapper Black wa Uswazi na Adam Juma
Akizungumza na Daladala Beat ya Megic FM jana, Black alisema atazidi kumheshimu Adam.
“Video hii ndio maana nikasema napendaga kufanya kitu kizuri kila
muda, sipendagi kufanya kitu kibaya, ndio maana najaribu bado kufikiria
nitafanya na nani, lakini siwezi kusema, najaribu kuangalia nitafanya na
nani video sasa hivi,” alisema.
‘Sidhani kama nitafanya na Adam Juma, lakini itavyokuwa itawezekana.
Kwa upande wangu mimi Adam Juma ni mtu wangu,kwa upande wangu mimi
siwezi kugombana na yule jamaa, nitazidi kum respect kama kawaida,
lakini labda kwa upande wake yeye, mimi kwangu kama itakuwa poa sawa
(nitafanya naYe video) mimi napenda iwe hivyo. Napenda tufanye issue za
maendeleo sio za beef.”

إرسال تعليق