
Na Bashir Nkoromo, Iringa
WAWAKILISHI
wa Chadema wakiongozwa na Mratibu wa Kampeni za chama hicho katika
uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Benson Kigaiya leo wameumbuka baada ya
kushindwa kuonyesha mbele ya jopo la Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC)
sheria ambayo wawakilishi hao wa Chadema waling’ang’ania kuwa ipo
kuwaruhusu wafuasi wa vyama kukaa mita mia kusubiri matokeo au kulinda
kura.
Chadema
walizidi kutahayari kiasi cha mwanasheria wa chama hicho, John Malya,
aliyeambatana wa wawakilishi hao, kwenye mkutano wa Tume na vyama vya
siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo utaofanyika Machi 16, mwaka huu, naye
kukiri kwamba hakuna sheria ambayo awali ilikuwa imedaiwa na Kigaia kuwa
ipo.
“Madai
haya ya kuwepo sheria inayoruhusu wafuasi au kundi la watu kukaa mita
mia kutoka kituo cha kupigia kura kwa lengo lolote ikiwepo kusubiri
matokeo au kulinda kura, yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na baadhi ya
vyama vya siasa, lakini nasi tumekuwa tukiwaambia kwamba hakuna sheria
hiyo, na kuwataka yeyote anayejua kifungu cha sheria hiyo atuonyeshe,
Kigaia wewe unasema ipo hebu tuonyeshe kifungu hicho”, alisema, Mjumbe
wa Tume hiyo Jaji Mstaafu John Mkwawa.
Mapema
Kigaia alisisitiza kuwa kwa upande wa Chadema wanaona kuwa sheria ipo
na kutokana na kuwepo sheria hiyo, kwa hiyo itakuwa ni haki ya msingi
kwa wafuasi wa chama hicho kukaa mita 100, wakisubiri matokeo ya kura
zao na pia kulinda ukiukwaji wowote unaoweza kufanyika kwa watu kutoa
rushwa au kupiga kampeni za chini chini wakati wa uchaguzi.
Maelezo
hayo ya Kigaia yalipingwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchguzi, Jaji
Mstaafu Damian Lubuva, akisema, sheria iliyopo ni inayotaka kuanzia mita
mia moja kutoka kituo cha kupigia kura pasiwepo nembo au ishara zozote
za utambulisho wa chama chochote kinachoshiriki uchaguzi.
Akitoa
taarifa ya Tume hiyo kwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ambavyo ni
CCM, Chadema na CHAUSTA, Mwenyekiti wa Tume, pamoja na mambo mengine,
alisema, mi marufuku kwa kundi au mtu yeyote kukaa kwenye kituo cha
kupigua kura au karibu na kituo hicho baada ya kupiga kura.
إرسال تعليق