Msanii wa Hip Hop, Darasa amewataka radhi mashabiki kwa
kuchelewa kutoka kwa filamu yake ya ‘Sikati Tamaa’ na kwamba ipo tayari
na itatoka.
Akizungumza na East Africa Radio jana, Darasa alisema filamu hiyo
imechelewa kutoka kutokana na watu waliotaka kuipeleka sokoni kushindwa
biashara.
“Baada ya kushindwa biashara na watu wa kwanza ambao walitaka
kuipeleka filamu sokoni,kuna watu ambao wanaishughulikia hiyo filamu na
makubaliano wakaniambia,’bwana una kitu kizuri zaidi cha kufanya na hiyo
filamu’ nafikiri walikuwa na mipango ya kuandaa event kubwa halafu hiyo
filamu izunduliwa kutokana na vitu ambavyo walinielewesha ni vitu
vizuri, mimi nikawaelewa nikaona niwaachie hilo swala na jukumu lote
lipo nikononi mwao,” alisema.
“Kitu ambacho nataka kuwaambia watu, mimi sio mtu wa kuamka
asubuhi na kwenda kusema kitu ambacho sijui hatima yake au sitakifanya
nilisema filamu itatoka, kutokana na makubaliano yetu ya mwanzo tulijua
kila kitu kitakuja kuwa rahisi ,but ikaja story tofauti ambayo ikatukata
ata ‘mood’ sisi. First time ya biashara watu wakatuambia wanataka
kutupa kiwango cha hela ambacho hatukukubaliana nacho sisi, so
haikutuingia sisi akilini ,so kitu ambacho nataka kusema kwa watu,ili
sisi tupate faida,tufanye makubaliano mazuri kati yetu na watu ambao
tutafanya nao biashara. Kwahiyo watu waombe Mungu tu, mimi still niko na
nitafanya vitu na hiyo filamu ni kitu ambacho kimefanyika kipo na
haiwezi kukaa ndani mwetu milele kitatoka, watu watusamehe kwa
disappointment ambayo imetokea. Hiyo ni moja na mbili niko studio
kwaajili ya kuhakikisha nafanya mambo mazuri,nataka kurudi kwenye game
na watu wanisubirie,” alisema Darassa

إرسال تعليق